Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, January 12, 2018

Mrema atoa taarifa polisi za kuzushiwa kifo

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania, Augustino Mrema amelitaka Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kumchukulia hatua aliyezusha taarifa za kifo chake Januari 9 mwaka huu.

Mrema ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Taifa ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya Kituo cha Polisi jijini Dar es Salaam alipokwenda kuripoti tukio hilo.

Amesema, aliyezusha taarifa hiyo alifahamu kwamba Lowassa amekwenda Ikulu kuonana na Rais Dkt Magufuli, hivyo akazusha uongo ili watu wasiwe makini kuhusu kilichojadiliwa Ikulu.

Mrema amesema wapinzani wa Rais ndio walizusha taarifa hizo za uongo na kuzua taharuki kwa sababu yeye ni mtu maarufu na wanajua kwamba kwa kufanya hivyo wangesababisha watu kutofautilia kilichozungumza Ikulu.

Baada ya kusema hayo, Mrema ameweka wazi kwamba anataka kulipwa fidia ya TZS 20 bilioni kutokana na kuzushiwa kifo na kwamba fedha hiyo haitapungua hata shilingi mia.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )