Thursday, January 11, 2018

Musukuma awavaa Chadema, asema hawana ubavu wa kumfukuza Lowassa

Mbunge wa Geita, Joseph Msukuma amesema kwamba viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wanapiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Lowassa kwenda Ikulu lakini hawana mabavu ya kumfukuza uanachama kwani yeye ndiye mwenye chama.

Msukuma amedai kwamba, Mbowe ambaye anaaminiwa kuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA tayari alikwishauza chama kwa Lowassa muda mrefu ndiyo maana hana sauti ya kumuwajibisha.

Aidha Msukuma hajaishia hapo ambapo pia amemtaka Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho aoneshe nguvu yake ndani ya chama kwa kumwambia Lowassa aombe radhi  na siyo waombane wao kwa wao kwani kutakuwa ni kuwapumbaza wanachama na wafusi wao bali hadharani watu waone.

"Lowassa ndiye mwenye Chama. Wewe mbowe uliuza chama sasa wewe kama msemaji toa kauli ya kumfukuza chama Lowassa. Tunashangaa kuanza kuchafuliwa kwa mtu ambaye mlituaminisha kuwa anafaa kuwa Rais. Muite Lowassa umhoji mitandaoni tuone akikuomba radhi. Na hata akikuomba radhi sasa hivi tutajua siyo kwa mapenzi yake," Msukuma.

Ameongeza kuwa, "Mbowe kusema kuwa Lowassa alikurupuka ni kumkosea adabu kwanza, Lowassa ni mtu mzima kwake na yeye bado ni kijana. Na  ninaamini kwamba wewe Mbowe Lowassa hakuombi msamaha kwa kuwa yeye ndiye mmiliki".

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )