Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 3, 2018

Mwakyembe Atoa Maagizo Mazito TFF

adv1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka TFF kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayohusu michezo ya ligi daraja la kwanza, kati ya Dodoma FC vs Alliance na Pamba vs Biashara.

Sakata la maamuzi yasiyo ya haki katika michezo ya Dodoma FC dhidi Alliance ya Mwanza na Pamba ya Mwanza dhidi Biashara ya Musoma ndio limefanya Waziri mwenye dhamana ya michezo kutoa agizo hilo kwa shirikisho ili kuhakikisha utata huo unamalizika.

Katika taarifa yake  Waziri Mwakyembe ameeleza kusikitishwa na malalamiko ya vitendo vya uonevu na upendeleo katika maamuzi ya mechi hizo huku TFF ikiwa kimya bila kutoa ufafanuzi wa maamuzi hayo.

Mechi hizo zilipigwa Disemba 30 maamuzi yake kugubikwa na utata mkubwa hivyo Waziri amemtaka Rais wa TFF Wallace Karia na viongozi wengine wahusika kuchukua hatua za kuchunguza maamuzi hayo na kuchukua hatua
.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )