Wednesday, January 3, 2018

Ray C Atoa Kali Ya Mwaka.....Amuomba Rais Magufuli Awabane Wanaume Wanaowachezea Bila Kuwaoa

Msanii  Ray C amefunguka na kumuomba Rais Magufuli asaidie kupatikana sheria ambayo itaweza kusaidia wanawake na mabinti wa Tanzania kuolewa kwa haraka kwani anadai bila wanaume kulazimishwa wataendelea kuwachezea mabinti tu.

Ray C amedai kuwa endapo kukiwa na sheria ya kuzuia mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke kabla ya ndoa itasaidia sana wanaume kuoa na kupelekea tatizo la mabinti kutoolewa kupungua.

"Mzee mimi na shida moja, hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji sana! Ombi langu la mwaka huu kwako ni hili. Naomba upitishe sheria hakuna mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume mpaka wafunge ndoa! Na yeyote atakaekutwa na mwanamke iwe hotelini! Guest house bila cheti cha ndoa wapelekwe wote Segerea. Nadhani itasaidia sana wanawake wengi kuolewa badala ya kuwa manungaembe" alisema Ray C

 Ray C amesema kuwa ameamua kuomba jambo hilo kwa kuwa amekuwa akishuhudia wanawake wengi wakiishia kuchezewa na kuachwa pasipo kuolewa lakini anadai kama kukiwa na sheria hiyo wanaume watakuwa na nidhamu na kunyooka maana watalazika kuoa tu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )