Loading...

Monday, January 29, 2018

Simba Mwendo Wa 4G.....,Okwi Mbili,Bocco Mbili

Timu ya Simba imezidi kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kupata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Majimaji kutoka Songea mkoani Ruvuma Mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa na kuhitimisha Mzunguko wa Kwanza.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa John Bocco dakika ya 17 akimalizia mpira uliorudi baada ya kugonga mwamba kufuatia beki Mghana, Asante Kwasi kupiga tik tak kuunganisha kona ya winga Shiza Ramadhani Kichuya.

Bocco aliye katika msimu wake wa kwanza Msimbazi tangu asajiliwe kutoka Azam FC , aliwainua vitini wapenzi wa Simba kwa kufunga bao la pili dakika ya 26 kwa kichwa akimalizia ‘majaro’ ya kiungo Said Hamisi Ndemla.

Hadi timu zinakwenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa magoli hayo mawili dhidi ya Majimaji kipindi cha pili kilianza kwa mabenchi yote ya ufundi kufanya mabadiliko hata hivyo yaliwanufaisha wenyeji zaidi.

Mnamo dakika ya 52 na 68 Simba walipata magoli hayo mawili kupitia kwa Mshambuliaji hatari Raia wa Uganda Emanuel Okwi na kuendelea kukalia usukani wa wafungaji akiwa na jumla ya magoli 12.

Kwa Matokeo hayo Simba wamefikisha Jumla ya pointi 35 huku wakifuatiwa na Azama 30 na mahasimu wao wakubwa wa jadi Yanga wakiwa kwenye nafasi ya tatu kwa pointi 28 na Mchezo mwingine ulipigwa katika dimba la Namfua ambapo wenyeji Singida United wamefanikiwa kupata pointi tatu baada ya kuwafunga Tanzania Prinsons goli 1-0.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )