Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, February 7, 2018

Lipumba kufukuza Madiwani Wote wa CUF Dar es Salaam

Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF kwa upande wa Maalim Seif, Mbarala Maharagande amefunguka na kuweka wazi kuwa Profesa Lipumba pamoja na genge lake wamepanga njama kuwafukuza madiwani wote wa CUF Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari Mbarala Maharagande amesema kuwa Lipumba amepanga njama za kuwafukuza madiwani wa CUF Dar es Salaam wakiwepo wastahiki Meya kutokana na madiwani hao kutokuwa na ushirikiano na Lipumba na kundi lake.

"Lipumba amepanga njama za kutaka kuwafukuza uanachama madiwani kwa tiketi ya CUF-Chama cha Wananchi mkoa wa Dar es salaam; wakiwemo wastahiki Manaibu Meya, kutokana na madiwani hao kukataa kumsaidia msaliti Lipumba na genge lake katika kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni.

" Lipumba na watu wake wamejikuta katika wakati mgumu kwa uamuzi wao wa kusimamisha mgombea wakipingana na uamuzi wa UKAWA wa kusimamisha mgombea mmoja kutoka miongoni mwa vyama washirika. 

"Uamuzi huo wa Lipumba ambao umetafsiriwa kuwa ni mpango wa kutaka kuzigawa kura ili kuisadia CCM ishinde, umeshitukiwa na wananchi wa jimbo la Kinondoni na kusababisha kususiwa mikutano yao ya kampeni na wadau mbalimbali"

Mbali na hilo Maharagande amedai kuwa chama hicho kimejipanga vyema kukabiliana na njama hizo zinazotaka kufanywa na Profesa Ibrahim Lipumba

"Tayari jopo la wanasheria wa Chama (CUF TAASISI) wamejipanga kukabiliana na hujuma hiyo vilivyo. 

"Tutaendelea kutoa taarifa kwa wanachama wote na umma wa Watanzania kwa ujumla juu ya kila kinachoendelea kwa wakati muafaka. 

"Tunatoa wito kwa wanachama wote, wapenda mabadiliko na demokrasia kwa ujumla kuzidi kuwa wastahimilivu na kuongeza kasi ya ushiriki wa shughuli mbalimbali za CUF Taasisi katika hatua hizi za mwisho za kumalizana na Wasaliti wa Mabadiliko na Demokrasia nchini" alisisitiza
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )