Loading...

Tuesday, February 6, 2018

Rais Magufuli, Kikwete, na Lowassa walivyomzika Mzee Kingunge Kinondoni

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli jana February 5, 2018 wamemzika Mwanasiasa Mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika makaburi ya Kinondoni Jijini DSM shughuli iliyotanguliwa na ibada iliyofanyika nyumbani kwake

Kingunge alifariki Siku ya Ijumaa akiwa anapatiwa matibabu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambiliwa na mbwa nyumbani kwake Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamini Wiliam Mkapa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika ibada ya mwisho ya marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye Kaburi la marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )