Wednesday, February 28, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Saba ( 17 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 

‘MAMA NINAKUOMBA UNIPE BARAKA ZAKO ILI NIWEZE KUMUOKOA BABA YANGU’
‘NAKURUHUSU KWA MOYO MMOJA NA MWANANGU NITAKUPA MSAADA WA CHOCHOTE UTAKACHO KIHITAJI HATA NUSU YA NGUVU ZANGU NITAKUPA ILI BABA YAKO AWE HURU KWANI BADO NINAMPENDA SNA’
‘MAMA NIMEDHAMIRIA KUIANZISHA DUNIA MPYA NA YENYE KILA AINA YA NGUVU ZITAKAZO IPINGA MAMLAKA TULIYOPO JUU YETU’

ENDELEA
“Mazungumzo kati ya Hitlaer na mama yake ambaye ni Janet yaliendelea kwa usiri mkubwa huku mama yake akimfundisha mbinu ambazo zitamsaidia mwanae katika kuikamilisha kazi ya kumuokoa baba yake.Hitler alijipanda vizuri na kutokana ni mjukuu wa miongoni mwa Malaika wakubwa mbinguni aliweza kutumia kigezo hicho kushuka duniani bila ya kuhojiwa maswali mengi na walinzi wanao linda dunia ambayo ipo katika hali mbaya ya kuuguzwa moto.

Hitler akaaanza kufanya uchunguzi wake kwenye shimo kubwa la moto liitwalo KUZIMU lililo kusanya idadi kubwa ya watu walio tenda maovu,Ila katika kuzimu nako kumegawanyika madaraja ya mateso ambayo yapo saba.Na kila waliopo kwenye daraja moja wanatofautiana kwa adhabu na waliopo kwenye daraja la pili hivyo hivyo na kuendele mbele kiasi kwamba matendo yako ndio yanakuchagua uingie kwenye daraja lipi unalo stahili kuhukumiwa.Hitler akaendelea kufanya uchunguzi wake katika magereza yote saba ila hakufanikiwa kumuona baba yake ambaye kwa jinsi mama yake alivyo muelekeza sio rahisi kwake kushindwa kumtambua ila gafla Hitler akiwa kuzimu……”
“Sory Sir Eddy muda wa kipindi chako umeisha”
Madam Zena alizungumza huku akiwa ameshika vitabu vya somo la Kiswahili jambo lililo pelekea wanafunzi kuanza kuzomea wakikataa asiingie

“Jamani tutamalizia hii story yetu kesho”
“Ahhhh Sir EDDY endelea bwanaaa Kswahili bongo akawafundishe mabasha zakee”
Sauti mmoja ya kiume ikitokea nyuma ya darasa ilisikika na kumfanya madama Zena kuchungulia mlangoni huku sura yake ikiwa imekasirika
“Mwana idhaya nani aliye zungumza hayo maneno?”
“Si ninawauliza nyinyi watoto mulio laaniwa na wazazi wenu.Msio na haya mafirahuni wakubwa nyinyi munajua maana ya basha……..Ehhhhh au munavyo jiona nyinyi humu ndani kuna mwanaume aliye kamilika nyote si mashogaa”
Madam Zena alizidi kutokwa na maneno ya kejeli hadi ikafikia kipindi wanafunzi wa kiume wakaanza kuzungumza chini chini na neno lililo sikika kutoka nyuma ya darasa walipo kaa wanafunzi wengi wa kiume ni
“Shoga baba yako aliyekuzaa”
Nikabaki nimeshika mdomo kwani kwa jinsi madam Zena alivyo mweupe wa kujichubu taratibu nikamuona sura yake ikitawali  na wekundu kwa  mbli ulio tokana na hasira
“Nasema nyote tokeni nje mupige magoti”
Wanafunzi wote wakakaa kimya wakisikilizia nani aanze kwenda nje kupiga mogoti ila kadri muda unavyo zidi kwenda hakuna aliye simama kwenda nje
“Monitres nenda kamuite Headmaster na mwalimu wa nizamu”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )