Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, February 4, 2018

Waziri Mkuu: Serikali kuimarisha masoko ya mazao

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.

Taarifa iliyotolewa jana Februari 3, 2018  na ofisi ya Waziri Mkuu inaeleza kuwa ametoa kauli hiyo  Januari 2, 2018 wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.

Amesema kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.

“Kupitia Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija ya mazao wanayolima,” amesema.

Ametoa mfano zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.

Awali, ofisa mtendaji mkuu wa TMX, Godfrey Malekano amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa wamejipanga vyema kuanza minada ya mazao.

“Tutaanzia na zao la ufuta mwezi Mei, 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo,” amesema.

Amesema kufanikiwa kwa soko la bidhaa na mfumo wa stakabadhi ghalani kunategemea msaada wa Serikali, “Soko la bidhaa la Ethiopia linalotajwa sana kwa mafanikio limefikia malengo yake kutokana na mkono wa Serikali.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )