Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 1, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 17 na 18)

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 
  
“Mama kuna nini?”      
“Kuna nyaraka za serikali ambazo ni muhimu sana, zimeibiwa. Sijui nitafanya nini mimi”
Mama alizungumza kwa unyonge huku machozi yakimlenga lenga mikono yake akiwa ameiweka kichwani, hapo ndipo taratibu nikaanza kupata picha ya mtu ambaye alitoka kasi na nilimuhisi kwamba ni mwaume wa Yudia kumbe sivyo hivyo ni mwanaume aliye kuja kuiba nyaraka muhimu za mama.
“Dany mwanangu unatakiwa kufanya kitu, la sivyo kazi sina mwanaungu”
Mama alizungumza huku machozi yakimwagika kitendo kilicho nifanya nijisikie vibaya sana moyoni mwangu.
  
ENDELEA
Kwa ishara nikamuomba Yudia kutoka chumbani kwa mama, naye akafanya hivyo akiwa katika hali ya woga. Taratibu nikamshika mama na kumkalisha kitandani kwake.
“Nitafanya nini mwanagu, mkataba huo ni muhimu na kesho kutwa raisi anakuja Tanga na anahitaji kuweza kuusaini”
Mama alizungumza machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Ikanibidi kukaza roho kama mtoto wa kiume kuto kulia mbele ya mama yangu kwa maana, machozi yake yanaufanya mwili wangu wote kusisimkwa na kujihisi na mimi ninaweza kudondosha chozi muda na wakati wowote.
“Kwani mama kuna kitu watu ambao una bifu bifu nao?”
Mama akakaa kimya kwa muda, kisha akatingisha kichwa kuashiria kwamba kuna watu ambao ana ugomvi nao.
“Ni kina nani hao?”
“Kuna huyu meya mpya, wao nina uhakika kwamba ndio wanao winda hizi nyaraka, wanataka kuziteketeza ili mpango wa ujenzi wa bandari mpya usifanikiwe”

“Na huyo meya ana kaa wapi?”
“Raskazoni kule”
“Ok ngoja nianze kuifanya hivyo kazi muda huu, ila nina kuomba usilie sawa mama yangu”
“Sawa”
Nikamfuta mama machozi kwa kitambaa chake, kisha nikanyanyuka na kutoka chumbani humo. Nikakutana na Yudia kwenye kordo akiwa kama ni mtu mwenye wasiwasi na kitu fulani, ila sikutaka kumsemesha chochote kwa maana mambo ya muhimu ya mama yamesha haribika. Tukiwa hapo kwenye kordo tukasikia sauti ya kungele ya getini ikiita. Yudia kwa haraka akaondoka na mimi nikaingia chumbani kwangu.
Nikafungua kabati na kutoa begi langu la nguo, nikaitoa bastola yangu, niliyo iweka chini kabisa ya nguo zangu, nikaitazama huku nikitoa magazine yake, nikaikuta ikiwa na risasi za kutosha na wala sijaitumia muda mrefu. Nikaiweka pembeni kisha nikatoa suruali yangu ya jinzi nikaiweka pembeni, nikiwa katika hatua hizo nikasikia mlango ukigongwa, kwa haraka nikaichukua basola yangu na kuirudisha ndani ya begi na kwa mwendo wa taratibu nikaelekea mlangoni na kuufungua.

“Kaka Dany daktari amesha fika”
“Nakuja”
Nikaufunga mlango mara baada ya Yudia kumaliza kunipatia ujumbe wake, nikalifunga begi vizuri na kutoka chumbani kwangu nikakutana na daktari ambaye mama alizungumza naye muda mchache ulio pita, nikamsalimia kutokna ni mzee wa makamo ya kina mama.
“Muheshimiwa yupo wapi?”
“Amejipumzisha mama, unaweza ukaanza kunihudumia tu”
“Ok sawa ninakuomba nione kidonda chako”
Taratibu nikavua shati na kumuonyesha daktari Kidonda hicho.
“Kimeanza kukauka”
Alizungumza, huku akikigusa gusa kwa juu. Akafungua kiji begi chake kidogo cha mkononi, akatoa kichupa kidogo pamoja na bomba la sindano lililo jipya kabisa.

“Nitakuchoma sindano ya kukikausha ndani ya siku mbili hizi kitakuwa kimepona kabisa”
“Ina maana na ngozi yake itarudi kama kawaida?”
“Hapana ngozi itarudi taratibu taratibu”
“Sawa”
Akachukua pamba na kuipaka dawa ya kusafishia, kwenye mshipa wa mkono wa kushoto. Alipo maliza kufanya hivyo akanichoma sindano hiyo yenye dawa ambayo nilisha wahi kuchomwa hospitalini juzi.
“Kijana unaonekana unafanya sana mazoezi”
“Kwa nini?”
“Mishipa yako imejitokeza kiurahisi ni tofauti sana na watu wengine mishipa yao kujitokeza ni kazi sana”
“Ahaaa, huwa na fanya sana mazoezi”
Daktari akachomoa sindano yake baada ya kuisukuma damu taratibu. Akanipatia pamba iliyo na dawa nikajiziba nayo katika eneo ambalo amenichoma sindano.
“Kesho asubuhi ukija Hospitalini kwangu nitakuchoma nyingine ya kumalizia”

“Sawa sawa hospitali yako ipo eneo gani?”
“Barabara ya pili pale”
“Ahaa ok asante”
Nikamuga daktari huyo na kuingia chumbani kwangu, nikafungua begi langu na kuitoa bastola kisha nikavua pensi na kuvaa jinzi, sikuona haja ya kulivua shati nililo livaa. Nikaichomeka bastola yangu kiunoni kwa nyuma na kutoka chumbani kwangu. Nikaingia jikoni kwa ajili ya kunywa maji kabla sijaanza upelelezi wangu wa kuifwatilia nyumba ya meya ambaye mama anamtilia mashaka.
Nikiwa hapo simu ya Yudia ikaingia mesiji, mwenyewe hakuwepo nikaona bora niichukue na ili kuifungua meseji hiyo niliyo hisi labda ni mtu ambaye ni bwana wake.
(Mambo yameharibika, kaeni kwa tahadhari mjulisheni na meya)
Meseji hiyo ameituma Yudia kwenda kwa mtu huyo aliye jibu ‘SAWA’. Nilijikuta nikianza kupata mashaka makubwa, kwa haraka nikaituma namba ya mtumaji wa meseji hiyo kwenye simu yangu, nilipo hakikisha kwamba nimemaliza kuituma. Nikaifuta meseji yake aliyo tuma na niliyo jitumia na simu ya Yudia nikairudisha sehemu nilipo itoa, nikatoka jikoni humo nikiwa nimejikausha na nikamkuta Yudia akingia kwenye mlango wa sebleni akitokea nje.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )