Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, March 3, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 19 na 20)

adv1
 MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 
“Ni upumbavu mulio fanya, munge muua. Sasa hii ni nafasi ya mwisho jifiche kwenye hiyo bustani wanarudi muda si mrefu. Sasa ole wako ufanye makosa nitakuua”
Maneno ya Yudia yalinifanya niishiwe nguvu kabisa kwa maana yale mawazo mabaya niliyo kuwa nina muwazia kumbe ni kweli na yeye ndio anahusika na mpango wa mauaji ya mama, nikatamani kuingia ila nilihisi kushindwa kabisa kwa maana jamaa huyo amejificha katika uwa kubwa lililopo kwenye bustani iliyopo karibu na getini na yoyote atakaye ingia ndani hapo ni rahisi kumuona ila mtu anaye ingia si rahisi kuweza kumuona muuaji huyo.

ENDELEA  
Nikashusha pumzi na kujiweka sawa huku macho yangu yakichungulia getini, nikamuona Yudia akiingia ndani na kuufunga mlango.  Nikasimama getini kama dakika mbili nikitafakari nini cha kufanya, nikautazama ukuta wa nyumaba yetu, kusema kweli siwezi kuupanda kwa maana juu umewekwa nyaya za umeme ambazo endapo mtu atapanda basi atakacho kutana nacho hapo ni shoti ya uhakika ambayo inaweza kupelekea hata akapoteza maisha.

Kutokana leo haturudi nyumbani, moja kwa moja nikaondoka getini na kurudi kwenye baa ambayo niliacha gari, nikaingia kwenye gari na kuitoa simu yangu mfukoni na kuanza kukagua taarifa alizo nitumia Joseph. Nikatoa na hati ya kusafiria ya gaidi niliye muua kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort, hapo ndipo nilipo gundua kwamba kuna kikundi kikubwa cha hawa magaidi kimeingia hapa jijini Tanga. Kwa maana niliye muua na huyu niliye tumiwa taarifa zake pamoja na picha yake ni watu wawili tofauti.
‘Sasa raisi anakuja Tanga inakuwaje?’  
Nilijiuliza swali huku nikiendelea kutazama hati ya gaidi niliye muua. Nikatafuta namba ya Joseph kwenye simu yangu na kumpigia, simu yake ikaita kwa muda kisha akapokea.
“Dany niambie”

“Poa hivi umesema raisi anakuja Tanga?”
“Ndio na tayari jamaa wamesha tumwa kuweka mazingira sawa”
“Nani ni mkuu wa upelelezi aliye fika Tanga?”
“Mzee Haule ndio anaongoza upelelezi na ulinzi mzima wa raisi”
“Ok nipatie namba yake niwasiliane naye, kwa maana kuna mfumo mbaya unakwenda kutokea”
“Vipi kuna hali yoyote ya hatari?”
“Ndio, nitumie namba yake niweze kuzungumza naye”
“Ok dakika moja ndugu yangu”
Nikakata simu na kuisubiria meseji ya Joseph, haikupita hata dakika meseji ikaingia kwenye simu yangu, nikaifungua kwa haraka na kukuta namba ya simu ya Mzee Haule, kwa haraka nikaipiga namba hiyo ya simu ambayo ikaita kwa muda kisha ikapokelewa na nikasikia sauti nzito yam zee huyo ambaye ninamfahamu kwa kumuona.

“Shikamoo mkuu”
“Marahaba, nani mwanzangu?”
“Unazungumza na Agent Daniel 008 kutoka kitengo cha N.S.S”
“Ndio”  
“Nipo mkoa wa Tanga kwa sasa likizo ila nina taarifa muhimu ambazo ninahitaji kuweza kuzileta kwako”
“Upo wapi kwa sasa?”
“Nipo maeneo ya Chumbageni”
“Ok unaweza kufika maeneo ya Tanha Hoteli hapa hapa Chumbageni”
“Kwenye hiyo hoteli?”
“Ndio”
“Dakika tatu nitakuwa hapo”

Nikakata simu na kuwasha gari, nikaondoka katika eneo hili, kutokana sio mbali sana na sehemu nilipo kuwepo, ndani ya dakika tatu nikawa nimesha fika katika eneo hilo. Nikashuka kwenye gari na kutoa simu yangu nikampigia mzee Haule aliye toka nje ya hoteli hiyo, akaingia kwenye gari langu na nikaanza kumpa taarifa muhimu sana za kuimarisha ulinzi.
“Ina maana wewe ndio uliye weza kumuua yule gaidi kule hotelini?”
“Sikumuua ila alijiua mwenyewe kwa kuhofia kutoa siri za watu wanao walio mtu hiyo kazi. Na hivi ndio vitu ambavyo niliweza kuvipata kama vidhibitisho”
Mzee Haule akapokea hati ya kusafiria ya gaidi huyo pamoja na waleti ambayo nilimpatia nyenye vikara vilivyo andikwa kwa lugha ya kiarabu. Mzee Haula akaanza kuzivizsoma, sura yake nikaona jinsi inavyo badilika, sikujua kama anaweza kuelewa lugha hiyo.


adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )