Sunday, March 4, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 21 na 22)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                     
ILIPOISHIA  
Nikasimamisha gari pembeni ya ukuta wa nyumbani kisha nikashuka kwa haraka na kuanza kukimbilia getini, nikafungua geti na kuingia ndani. Sikuamini macho yangu kuwakuta wale askari ambao niliwaacha muda mchache tu ulio pita. Sasa hivi wote wawili wamelala chini wakiwa wanavuja damu ikionyesha kwamba wameuwawa. Nikiwa katika kushangaa shangaa, mlango wa kuingilia sebleni ukafunguliwa, uso kwa uso nikakutana na Yudia aliye shika begi lake mkononi akionekana yupo kwenye harakati za kutoroka huku nyumbani kwetu
      
ENDELEA
Kwa haraka nikaichoma bastola yangu na kumuelekezea Yudia ambaye amebaki akiwa amesimama na kunikazia macho, akawatazama askari alio waua, kisha akayarudisha macho yangu kwangu. Akalitupa begi lake chini akiashiria kwamba yupo tayari kwa mapambano. Akaanza kunifwata kwa kasi huku akinitazama sikutaka kumpiga risasi lengo langu kubwa ni kumkamata akiwa hai. Alipo nisogelea karibu nikaruka hewani na kumtandika teke la kifua lililo mrudisha nyuma na kumuangusha chini. Nahisi Yudia hakuweza kunifahamu vizuri, alihisi mimi ni mtu wa kawaida kawaida sana lakini sivyo, kwa maana tama yangno nimesha ikweka mbeni na sasa hivi ninacho kijali ni kazi yangu ya kulitumikia taifa langu.

Yudia akajizoa joa chini na kunyanyuka, akajidai kukunja ngumi, nikamtazama kwa macho makali yaliyo jaa hasira, akajaribu kurusha ngumi kadhaa ila zote nikazikwepa na kumtandika ngumi ya shingo iliyo myumbisha na kumungusha chini. Kwa haraka akasiamam huku akitingisha kichwa chake akihitaki kujiweka sawa. Akarusha teke kwe mguu wa kulia, kwa kasi ya ajabu nikaupiga mguu wake wa kushotoi hata kabla mguu wake wa kulia haujafika chini. Anguko hili la sasa, likamfanya Judia kutoa kilio cha maumivu makali kwa maana amengukia mbavu zake.
Nikamsogelea kwa ukaribu huku bastola yangu ikiwa mkononi. Nikampapasa na kuitoa bastola yake aliyo ificha kwenye viatu, nikaanza kumburutu na kumuingiza hadi sebleni. Nikamburuza hadi chumbani kwake na kumtupia kitandani. Chumba chake kimechanguliwa changuliwa sana.
“Nahisi safari hii utanijibu kwamba wewe ni nani?”

“Fuc**……..”
Sikumpa nafasi ya kumalizia tusi lake, nikamtandika kofi zito la shavu hadi akamwagikwa na damu za mdomo.
“Wewe ni nani?”  
Yudia akaka kimya huku akinitumbulia macho, hakujibu chochote. Sikujali kama ni mwanamke au ana uzuri gani, nikamtandika ngumi nzito ya uso, iliyo mfanya apige ukunga mkali sana wa maumivu.
“Wewe ni nani?”
“Niueee tuu”
“Ahaa nikuue?”
“Ndioo”
Yudia alizungumza huku akilia, nikakoki bastola yangu na kuiweka sawa, nikavuta traiga na kuiruhusu risasi kutoka ikatua kwenye paja la Yudia na kumfanya apige ulelele mkali sana.
“Nimekuuliza wewe ni nani?”
Nilizungumza huku jasho likinimwagika uso mzima, sikuhitaji kufanya upuuzi mwingine kwa binti huyo. Damu nyingi zikasambaa kwenye shuka la kitandani, Yudia akanitazama kwa uchungu sana huku dhairi akionyesha kwamba ana hasira kali sana dhidi yangu.

“Wewe ni nani?”
“M…..i…i…mi ni……mwan…..an….a…..mgamb….oo wa Alsahab”
Yudia alizungumza huku akilia sana tena kwa uchungu mkali sana.
“Umefwata nini nyumbani kwa mama yangu?”
“N…ii nilitumwa kuja…..a kumpe….lelezaa”
“Nani kakuagiza?”
Hapo Yudia akaka kimya, nikaisogeza bastola yangu karibu kabisa na paji la uso wake huku mwili mzima ukinitetemeka kwa hasira kali sana
“NANI KAKUTUMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA”
Niliuzungumza kwa kufoka hadi Yudia akayafumba macho yake kwa maana sauyti yangu imetoka ikiwa na mtetemesho mzito wa hasira.
“Meya Meyaaaaa, ndio mzamini wa haya yote”
“Ahaaa lengo lake ni nini?”

“Kuu….kuuu muondoa raisi madarakani”
“Raisi madarakani!?”
“Ndio kuna kikundi tayari kipo nchini Tanzania, kipo tayari kujitoa muhanga kesho kutwa raisi akija hapa Tanga”
Hapo sasa ndipo nikaanza kupata picha ya haraka sana, wale watu nilio waona katika jumba lile la kifahari kumbe ndio wana mpango wa kumuua raisi.
“Dany naomba uniue kwa maana nimesha toa siri ya kundi langu ni lazima wataniua kiukatili mimi”
Yudia aliniomba huku akimwagikwa na machozi mengi usoni mwake. Sikutaka kabisa kufanya mauji ndani ya nyumba yetu. Nikampiga Yudia shingoni na kitako cha bastola yangu, kisha nikambeba begani na kutoka naye chumbani kwake. Moja kwa moja tukatoka nje, nikachukua begi lake la nguo na kuondoka eneo hilo.

KwA umakini wa hai ya juu nikatoka nje kabisa ya geti, baada ya kuchunguza kwamba hakuna watu wanao nifwatilia. Nikasogea hadi gari shemu lilipo nikamuingiza Yudia ndani ya gari pamoja na begi lake, kisha nikazunguka upande wa pili wa dereva nikaingia na kuondoka nyumbani. Akili yangu kwa haraka ikanituma kwa daktari aliye kuja kunitibu leo. Kutokana alisha nielekeza sehemu ilipo hospitali yake moja kwa moja nikaeleka hadi kwenye hospitali yake japo ni usiku ila nimedhamiria kufika katika eneo hilo.
Nimatoa Yudia ndani ya gari na kuuingia naye ndani ya hospitali hiyo, nikakutana na nesi akiwa mapokezi ana sinzia sinzia.

“Nimemkuta daktari?”
Sauti yangu ikamstua nesi huyo aliye jikuta akikurupuka na kunitazama. Akamtaza Yudia niliye mbeba begani.
“Yupo wapi daktari”  
Nilimuuliza kwa ukakali, pasipo kunijibu chochote kwa ishara akanionyesha eneo la kuingia ambapo ndipo kwa daktari. Nikaelekea katika chumba hicho cha dkatari, pasipo kubisha hodi nikaufungua mlango huo na kumkuta dokta aliye kuja kunitibu nyumbani akiwa amekaa kwenye kiti huku mbele yake kukiwa na meza kubwa. Alipo niona akavua miwani yake na kunyanyuka na kunisogele.
“Muweke hapo kwenye kitanda”  
Alizungumza huku akinionyesha kitanda ambacho kipo hapo kwenye ofisi yake huku kikiwa kimezungushiwa shuka kubwa la kijani. Nikamlaza Yudia chali na kumuweka vizuri.

 
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )