Saturday, March 10, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 33 na 34 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 

Kutokana sikuwa nimekaa sehemu yoyote nikageuza na kutoa chumba huku nikiufunga mlango wa chumba vizuri. Nikaanza kutembea kwenye kordo hii huku nikiwa makini kutazama nyuma na mbele. Mlango wa chumbani cha mbele ukafunguliwa, ikanibidi kupunguza mwendo  wa kutembea, macho yakanitoka baada ya kumuona K2 na Lukas wamesimama mlangoni hapo huku wakipigana mabusu ya mdomoni, huku Lukas akiwa amejifunga taulo kiunoni na K2 akiwa amevalia suti yeusi, ila vifungo vya shati lake vikiwa havikajaa vizuri, kwa bahati mbaya, K2 akanitazama, kitu kilicho mstua sana hata Lukas naye alivyo niona akakimbilia ndani.
  
ENDELEA  
Nikamtazama K2 kwa macho makali yaliyo jaa hasira. Sikutaka kumsemesha chochote zaidi ya kumpita na kuanza kushuka kwenye ngazi kwa kasi.
“Dany, Dany”
Niliisikia sauti ya K2 ikiniita kwa nyuma yangu, sikuona haja ya mimi kuweza kusimama, zaidi ya kuendelea kushuka kwneye ngazi.
“Dany nakuamrisha kama bosi wako, simama”
Kauli ya K2 ikanifanya nigeuke taratibu na kumtazama kwa macho yaliyo jaa dharau, nikamtazama jinsi anavyo hema kwa kuchoka kwa kukunikimbiza, kwenye ngazi hizi.
“Ndio bosi”
“Dany umefikaje fikaje huku?”
“Hicho ndicho kilicho kufanya unisimamishe?”
“Ahaa… kwa maana wewe unaumwa?”
“Kwa hiyo?”
“Sio vizuri kutembea tembea”
“Ehee”
“Ndio”
“Ok”
Nikaanza kushuka tena kwenye ngazi na kumfanya K2 kuniwahi na kunishika mkono wangu wa kulia, nikageuka kwa haraka huku mkono wake nikiwa nimeachanisha kwa nguvu na mkono wangu.
“Hembu nisikilize wewe malaya usiye jitambua. Cheo chako unakitumia katika kutembea na vijana si ndio?”
Nilimfokea K2 hadi akarudi nyuma huku  akiwa amenitumbulia macho ya woga sana.
“Upumbavu wako wote ulio kuwa unaufanya, na hichi nilicho kiona leo nimeutambua. Sasa mwisho uwe leo sihitaji mauhusiano na wewe tena. Umenielewa?”

Nilizungumza kwa sauti nzito huku tinda za sura yangu zikiwa zimejikunja kisawa sawa. K2 hakuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kukaa kimya, woga ukiwa umemjaa. Nikaanza kushuka kwneye ngazi huku nikiwa nimejawa na hasira kali, K2 hakuthubutu hata kunyanyua mguu wake na kunigfwata, nikafika mapokezi na kumkuta msichana ambaye ni muhudumu wa hii hoteli.
“Nahitaji maji makubwa na mzinga wa Vodka”
“Sawa”
Dada huyo akafungua friji kubwa lililopo nyuma yake na kunikabidhi chupa kubwa ya maji, kisha akanipatia na mzinga huo wa Vodka.
“Naweza Kulipa kwa creadit card?”
“Ndio”
Nikatoa waleti yangu, na kuchomoa kadi ya malipo, akaipisha kwneye mashine moja ya kulipa kisha akanirudishia kadi yangu, taratibu nikaanza kazi ya kuzipandisha ngazi hizo nikielekea gorofani. Sikumkuta K2 katika sehemu ambayo nilimuacha. Moja kwa moja nikaelekea katika chumba nilicho muacha Babyanka, nikafungua mlango wa chumba hichi na kuufunga kwa ndani.
“Hei nimerudi”

 
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )