Saturday, March 24, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 59 na 60 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA    

‘Sekunde nne’
Nilijiseme moyoni huku nikiingiza tena namba ya siri ambayo Marim aliniambia. Polisi walio kuwa wakinikimbiza nao wakasimama mbali na mimi kwa maana katika kufa hakuangalii kama wewe ni polisi au laa. Nikaiingiza tena namba ya siri aliyo niambia Marima ila nayo ikagoma jambo lililo nifanya nikate tamaa na nikabaki nikitazama sekunde mbili ziishe na tulipuke na kufia katika eneo hili

ENDELEA
Wazo moja likanijia kichwani mwangu, kwa haraka sikuhitaji kuweza kulizembea kirahisi. Nikaandika jina la nchi ya Somalia kwenye batani za hili bomu, nikayafumba macho yangu kusubiria kulipuka kwa bumu hili huku nikisali sala yangu ya mwisho. Sekunde ambazo nilikuwa ninazisubiria ili bumu kuweza kulipuka zikapita pasipo chochote kutokea. Taratibu nikayafumbua macho yangu nikakuta bomu hili limezima. Jasho mwili mzima linanishuka, watu wote uwanjani walibaki wakinitazama mimi huku wengi wao wakiwa wamekaa umbali mkubwa kutoka sehemu nilipo hata mpira ulisimamishwa kutokana na taharuki hiyo iliyo jitokeza hapa uwanjani.
Nikamuona Mariam kwa mbali akinipunga mkono huku akininyooshea kidole gumba cha mkono wa kulia. Polisi wakaanza kunisogelea huku wakiniomba ninyooshe mikono juu, siwezi kukimbia kwa maana karibia polisi wote wamenizunguka.

Mashabiki walipo ona polisi wanataka kunifunga pingu mikononi, wakaanza kupiga kelelele huku wakikimbilia eneo nililopo na polisi hawa.
Hiyo ndio ikawa nafasi kwangu kuwatoroka polisi huu kwa maana umati mkubwa wa mashabiki umewazuia wasinikamate. Moja kwa moja nikaelekea kwenye maegesho ya magari, nikiwa ninalitafuta gari langu sehemu nikastulia risasi ikipiga kwenye moja ya gari la pembeni hadi kioo cha gari hilo kikapasuka, kwa haraka nikachuchumaa chini, na kujibanza kwenye gari hilo. Nikamuona Yudia akiwa na vijana wawili wenye bastola wakinyata kwa uangalifu wakija sehemu nilipo. Kitendo cha kuchungulia nikastukia risasi nyngine ikipiga kwenye gari hili na kujikuta nikirudi kukaa chini sehemu nilipo jificha huku nikihema sana kwa wasiwasi.
“Wewe malaya jitokeze huwezi kuharibu mipango yetu”

Yudia alizungumza kwa ukali jambo lililo nifanya nizidi kukaa chini nikifikiria nini cha kufanya kwa manaa, sina silaha yoyote ambayo inaweza kuniwezesha kupambana nao. Wakaendelea kufyatua risasai mfululizo ambazo zinatoka kimya kimya kutokana na  viwambo vya kuzuia sauti walivyo vifunga kwenye risasi zao.
“Wewe malaya toka hapo chini lazima tukuue ku**ko”
Yudia akaendelea kurupoka, kwa bahati nzuri nikasikia milio ya risasi, katika kuchungulia nikaona polisi wakishambuliana na kina Yudia wakihakikisha kwamba wanawaweka kati. Sehemi nilipo sikuweza kujitoa kutokana na mirindimo hiyo ya risasi ambayo sikufahamu zinaelekea wapi.
“Wekeni mikono juu na bunduki pembeni”
Niliisikia sauti ya kiume ikizungumza kwa kuamrisha, taratibu nikajinyanyua na kuchungulia sehemu inapo tokea nikamuona Yudia pamoja na jamaa mwengien wakinyoosha mikono yao juu, huku mmoja akiwa amelala chini akivunjwa na damu.

“Heii na wewe nyanyuka”
Nilistuka sauti ya askari ikizungumza pembeni yangu, taratibu nikanyanyuka huku nikinyoosha mikono yangu juu. Yudia na mtu wake wakafungwa pingu, huku mimi nikiombwa kuongozana na askari wanne kuelekea katika chumba cha mahojiano ndani ya uwanja huu. Kutokana hakuna askari aliye weza kugundua kwamba mimi ni mwanaume, sikuweza kubisha nikaongozana nao hadi kwenye chumba cha mahujiano. Hapo nikakutana na mkuu wa askri wa upepelezi ambaye ninamfahamu vizuri japo yeye hanifahamu mimi. Askari walio niingiza kwenye chumba hichi wakatoka na kuniacha na mkuu  wao huyu.
“Binti unaitwa nani?”
“Lissa”
“Kwanza nitangulize shukrani zangu kwa kuweza kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania wengi katika huu uwanja. Pia…..”
Akanyamaza kimya baada ya simu yangu kuita, nikatazama ni nani anaye piga na kukuta ni mama ndio anaye piga, ikanibidi kupokea mbele ya mkuu huyu wa polisi  kitengo cha upelelezi.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )