Sunday, March 25, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 61 na 62 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA 

“Mwanamke nani?”  
Nilizungumza katika sauti yangu ya uhalisia, huku nikipandisha mikono yangu kwenye kifua chake na kuendelea kuzitomasa chuchu zake. Nikamgeuza na kuanza kumnyonya denda, taratibu Babyanka akaanza kuvua koti lake la suti, huku mimi nikiwa na kazi ya kumfungua vifungo vya shati lake jeupe alilo livaa. Tukiwa katika mahaba mazito gafla dirishani likaingizwa bomu la machozi lililo anza kutoa moshi mzito ulio tufanya tuanze kukohoa, hata hatujakaa vizuri taa za chumba chetu zikazima na kuanza kusikia vioo vikipasuka na kuanguka kwenye sakafu jambo lililo zidi kutuchanganya mimi na Babyanka
  
ENDELEA  
Kwa haraka tukakimbilia bafuni, kitendo cha kuingia nikawahi koki ya bomba na kufungulia maji mengi na  kuanza kunawa nyuso zetu kukata sumu ya bomu hili la machozi linalo fanya mtu mwagikwe na machozi na hata mbele usione.
“Chukua”
Babyanka alizungumza huku akinipatia basolola, nikaishika vizuri tayari kwa mashambulizo yoyote yatakayo tokea. Tukajibanza kila mtu kwenye kona yake ya ukuta wa mlango tulio uweka kati na upo wazi. Japo kuna giza ila tupoa makini sana kuhakikisha kwamba kila kitu kinacho kuja mbele yetu tunakisambaratisha.
Tukaona miyale myekundu myembaba inayo fungwa kwenye bundiki maalumu, ikikatisha katisha ndani ya chumba. Kutokana hatuonani na Babyanka tukashindwa kabisa kupeana ishara, kitu ambacho tunatakiwa kukifanya sasa hivi ni kuhakikisha kwamba tunashambulia tu.

Mlio wa simu yangu uliyopo chumbani kwenye kipochi changu ndio ulio wapotezea umakini watu hawa wanao tuwinda, tulicho kifanya ni kuaza kufanyatua risasi mfululizo kuelekea walipo watu hawa ambao idadi yao wapo sita.
Miguno ya maumivu ndio ilisikika ikiambatana na vishindo vizito vya watu kuanguka. Ndani ya dakika mbili ukimya mkali ukatawala ndani ya humba huku bunduki zote zenye myale hii myekundu zikiwa zimelala chini.
“Psiii”
Babyanka aliita kwa sauti hiyo ya chini, taratinu nikamuona akiingia kwenye chumba akiwafwata watu hawa tulio waua, hata mimi nikamfwata kwa nyuma. Mlango wa hapa hotelini umefunguliwa, kwa haraka nikaufungua taratibu na kuchungulia kwenye kordo sikumuona mtu yoyote. Babyanka naye akachungulia kwenye dirisha hakumuona mtu wa aina yoyote.
“Ni kina nani hawa?”
Niliuliza huku nikiufunga mlango
“Sifahamu, ila hii sehemu sio salama kabisa”
Nikatafuta kipochi changu na kutoa simu yangu, nikawasha mwanga wa tochi iliyopo kwenye hii simu yangu na kuanza kuwamulika majambazi hawa walio valia vitambaa vyeusi machoni mwao na kubakisha macho tu.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )