Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, March 16, 2018

Jeshi la Polisi Latoa Taarifa Kuokotwa Mwili wa Mmiliki wa Mabasi ya Super Sami Ukiwa Kwenye Kiroba

Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Mara, limetoa taarifa rasmi juu ya kuokotwa kwa mwili wa mfanya biashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah , ambaye alitoweka na mwili wake kuokotwa mtoni hapo juzi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Jafari Mohamedi, amesema hapo Jumatano walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuokotwa kwa kiroba chenye mwili ndani, na walipokifungua na kuita watu kutambua, ndipo alipojulikana kuwa ni mwili wa mfanya biashara huyo anayeishi mkoani Mwanza.

"Jumatano jioni  tumeweza kupata mwili wa marehemu huyu Samson Josiah ambaye ni mmiliki wa mabasi ya Super Sammy anayeishi Mwanza

"Tulipata taarifa  kwamba kuna mwili umeonekana katika mto ambao unatenganisha mkoa wa Mara na mkoa wa Simiyu unaoelekea mbugani Serengeti, wananchi waliona kiroba kimefungwa kinaelea, kikavutwa wakajulishwa polisi kufungua ndani wakakuta mwili wa marehemu.

" Kwa sababu tulikuwa na taarifa za utafutaji na mashaka juu ya kutoweka kwake, tukajulisha ndugu hao na wakatambua mwili wa marehemu”, amesema Kamanda Mohamedi.

Kamanda Mohamedi aliendelea kwa kueleza kwamba marehemu alitoweka kuanzia tarehe 27 mwezi wa pili ambapo aliondoka mkoani mwanza, na ndugu zake walisema kuwa aliaga anaenda Simiyu kwa shughuli zake za kibiashara na kuna mtu anamdai na akapotea tangu siku hiyo, na gari yake aliyotoka nayo Mwanza kukutwa imechomwa mtoto maeneo ya Serengeti mnamo tarehe 8 hadi kuteketea kabisa.

Imeelezwa kwamba kwa sasa mwili huo umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya postmoterm, na baadaye utatolewa kwenda kuzikwa, na mpaka sasa watu wanne wameshikiliwa kufuatia tukio hilo, upelelezi bado unaendelea
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )