Monday, March 12, 2018

Kisa picha ya Mwanae,Mama Kanumba Amwaga Machozi Standi.

Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba ameshangaza wengi baada ya kuanza kumwaga machozi  katika moja ya stand zinazojaza watu jijini dar baada ya kuona bango lenye picha ya mtoto wake katika maeneo hayo.

Mama huyo ambae alishindwa kuzia hasira zake na kulia alisema kuwa mara nyingi amekuwa akiumia sana na kushindwa kujizuia kutoa machozi kila  anapoona picha au kitu chochote ambacho kinamkumbusha mtoto wake.

"Kila mara nimekuwa nikiziona picha za kanumba katika mabango , lakini sijui kwanini hii imenifanya nipatwe na uchungu na niishiwe na nguvu kabisa.-Alisema Mama Kanumba ambae anasema kuwa alikuwa akielekea maeneo ya segerea kwa ajili ya kyrekodi movie.

Kanumba alifariki miaka zaidi yamitano iliyopita baada ya kuuawa na mpenzi wake (Lulu Michae) waliokuwa na mtafaruku na kusababisha mauaji yake pindi walipokuwa wakizozana.Hata hivyo Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baaada ya kukuta na hatia ya kuua bila kukusudia.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )