Friday, March 23, 2018

Lady Jay Dee asema kulia sasa basi....Atambulisha Wimbo Mpya wa ANAWEZA

Msanii  wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura, maarufu "Lady Jay Dee" ameendelea kuonyesha ukongwe wake katika sanaa hiyo baada ya jana kutambulisha kibao chake kipya kiitwacho Anaweza.

Lady Jay Dee au Komando ameutambulisha wimbo huo sambamba na kutoa video ili kuwavuta karibu mashabiki wake ambao wanafahamu kiwango chake.

Lady Jay Dee, alisema kuwa kibao hicho kitengenezwa na mtayarishaji Spicy Judoka wa Nigeria huku video ikisimamiwa na Justin Compus Lutona wa Afrika ya Kusini na lengo la kuchanganya wataalamu hao ni kuhakikisha kazi yake inakuwa na hadhi ya kimataifa.

Alisema kuwa baada ya kukamilisha kazi hiyo, anajiandaa kufanya onyesho la muziki na tayari ameanza maandalizi kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki wake.

Aliwataja wasanii wengine ambao wanamuunga mkono kuwa ni Rutta Bushoke, Nikki Mbishi na Judoka anayeimba muziki wa Hip Hop na kueleza kuwa nyota wengine atawatangaza hapo baadaye.

“'Nimemiss' jukwaa, nimemiss watu wangu, nimemiss ile kazi ya kusimama masaa kadhaa na kuwasiliana na watu wanaounga mkono muziki wangu kwa miaka nenda, rudi.

Nimeamua sasa kuwa nitafanya haya matamasha mara kwa mara ili mwisho wa siku muziki wangu uendelee kuishi miongoni mwa mashabiki wangu kwa sababu tukisema ukweli ndio kitu ninachokipenda, muziki”, alisema Lady Jay Dee ambaye ana albamu saba.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )