Monday, March 26, 2018

Maalim Seif asema Waraka wa Maaskofu KKKT Umemfariji

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amelipongeza Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kutoa waraka mzito wa ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka.

Waraka huo ulitolewa mwishoni wa wiki iliyopita ambao mbali na kuzungumzia masuala ya kiroho, umetaja changamoto tatu na kuzifikisha kwa waumini wake “ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.”

Changamoto zilizotajwa katika waraka huo uliopewa jina la “Taifa Letu Amani Yetu” na kusainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini ni hali ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa na masuala mtambuka likiwamo suala la Katiba Mpya.

Akizungumza leo Machi 26, 2018 jijini Dar es salaam wakati akisoma maazimio manne ya Kamati ya Utendaji ya Taifa ya chama hicho iliyokutana leo, Maalim Seif amesema anafarijika kuona  viongozi wa dini  wanakemea mambo ambayo hayaendi sawa nchini.

"Nimefarijika kuona viongozi wa taasisi za dini wakizungumza pale ambao wanaona mambo hayaendi sawa. Tusitafsiri  kwamba wanafanya siasa, hapana ni haki yao kukemea, "amesema Maalim Seif.

Amesema angetamani kuona viongozi wengine wa dini  wakionyesha misimamo kama maaskofu hao.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )