Friday, March 23, 2018

Makonda Awaita Ofisini Kwake Wanawake Waliotelekezwa Na Waume Zao

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  amewataka wanawake wote waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto wafike ofisini  Jumatatu ya  Aprili 9 kwa lengo la  kupatiwa msaada wa kisheria.

Taarifa ya Makonda kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana amesema jopo la wataalamu wa sheria, maofisa ustawi wa jamii na askari Polisi kutoka dawati la jinsia wamejipanga ipasavyo kuwahudumia na kuhakikisha mzazi mwenza anatoa fedha kwa ajili ya matunzo ya mtoto.

"Huduma hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Tano.Ewe mwanamke huu si wakati wa kulia wala kuteseka kwani Serikali yako itasimama na wewe hadi upate haki yako," amesema Makonda.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )