Wednesday, March 21, 2018

Mfanyabiashara wa Kinondoni Kafikishwa Mahakamani Kwa Kusafiirisha Dawa za Kulevya

Mfanyabiashara, Hariri Mohammed Hariri (45), mkazi wa Kinondoni, jana alipandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu Tuhuma za kusafirisha zaidi ya gramu 214 za dawa za kulevya.
 
Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Clara Chalwe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi imedaiwa Machi 2 mwaka huu huko Kinondoni Matitu ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa alisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 214.11.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chohote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya  isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Na imeahirishwa hadi Aprili 4 mwaka huu
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )