Wednesday, March 21, 2018

Polisi Dodoma imewakamata watu wawili kwa kusambaza taarifa za maandamano ya April 26 2018.

Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limewakamata na kuwashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii yanayotarajiwa kufanyika April 26 mwaka huu.

Kamanda wa polisi wa mkoa Dodoma Gilles Muroto amesema watu hao wamekua wakisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kuandamana huku wakijua ni kosa kisheria.

Aidha Kamanda Mruto ametoa wito kwa watu kutofuata mkumbo kuhamasisha watu kufanya maandamano kwani ni kosa kisheria na kuwa yeyote ambaye atakamatwa atashughulikiwa kisheria.

"Watu hawa wamekuwa wakihamasisha wananchi kufanya maandamano, tulishasema Serikali haijalibiwi leo tunaanza kutoa mifano kwao. Wale wote wanaoijaribu Serikali tutahakikisha tunawachukulia hatua za hali ya juu sana”

Mbali na hilo Kamanda Mruto amesema kuwa upelelezi ukikamilika watu hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao kuhusu kuhamasisha watu kufanya maandamano kupitia mitandao ya kijamii ambayo yamepangwa kufanyika April 26, 2018 nchi nzima na yakiratibiwa na mwanadada Mange Kimambi kupitia mitandao ya kijamii.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )