Wednesday, March 28, 2018

Prof. Jay: Nimeshafanya Kolabo na Diamond, Bado Alikiba

Mwanamuziki mkongwe na mmoja kati ya waanzilishi wa muziki wa Bongo fleva, Joseph Haule au maarufu kama Profesa Jay ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi amekiri kuwakubali Diamond, Alikiba na mpango wake kwa sasa ni  kufanya Kolabo na Ali Kiba.

Huwezi kutaja wasanii wakali wakongwe Bongo ukamuacha Prof. Jay mchango wake ni mkubwa sana na michano yake mpaka leo bado ikipigwa lazima mtu utoe saluti.

Siku ya jana Professor Jay alifanya Interview na The Playlist ya Times Fm na alifunguka kuhusu wasanii anaowakubali kwa hivi sasa na Kwanza alimtaja Diamond na kusema kuwa anavutiwa sana na wimbo wake wa African beauty:

"African beauty ni wimbo ambao nimeupenda kwa sababu amemshirikisha Omarion halafu ameimba Kiswahili alafu mimi napenda kiwanja shabiki wa kuona wasanii International wanaimba kwa lugha yetu na kuitangaza nchi yetu”.

Lakini pia Profesa Jay ameongelea kuhusu kolabo aliyofanya ya ‘kIPI sijasikia’ ya Diamond na mipango yake ya kufanya na Alikiba:

"Kusema kweli nimeshafanya ngoma na Diamond na ni naona ulikuwa wimbo bora wa mwaka 2015 Kupitia tuzo za Kili awards lakini na Ali Kiba ni time tu haijafika kwa sababu juzi tu nilikuwa naongea na Tundaman akaniambia kuna kolabo tutafanya na Alikiba kwaiyo hiyo inakuja”.

Prof. Jay amesema alikuwa ana mpango wa kufanya naye Kolabo kwa muda mrefu na hana tatizo na Alikiba na anamkubali pia.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )