Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, March 1, 2018

Shilole ahukumiwa kulipa faini Milioni 14

Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam imemhukumu msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu Shilole kulipa faini ya kiasi cha shilingi milioni 14, baada ya kupatikana na hatia ya kutapeli na kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye tamasha.

Katika kesi hiyo imethibitika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha shilingi Milioni tatu na Mary Musa ambaye ndiye muandaaji wa shoo hiyo,  ili aweze kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka wa mwaka jana, 2017 katika ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam, lakini hakufika kama walivokuwa wamekubaliana.

Baada ya mashabiki waliokuwa wameahidiwa kupata burudani kutoka kwa Shilole kutokumuona, walipandwa na hasira na kufanya vurugu kubwa iliyosababisha uharibifu wa mali za thamani ya shilingi milioni 14.

Kutokana na kitendo hicho, Mahakama imemuamuru Shilole kulipa kiasi hicho cha fedha kama fidia kwa mlalamikaji ambaye ni Mary Musa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )