Sunday, March 25, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini ( 40 )


AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Nikakimbilia ndani na kwenda moja kwa moja nikaingia chumba alipo mtoto,Sikuyaamini macho yangu kwani nilimkuta amekuwa mkubwa na kufikia ukubwa babu mtu mzima mwenye mandevu mengi na anatisha kupita maelezo,akanitazama kwa jicho lake kililo kubwa kama gololi za kuchezea pooltable
“NATAKA DAMU YAKO”

ENDELEA
Nikabaki nikiwa nimesimama kama ninasubiri kupapigwa picha ya mnato,kukimbia ninataka ila miguu inashindwa,Nikajikuta nikitabasamu kama mtu aliye pumua kwa njia ya haja kubwa mbele ya mama mkwe.Likasimama na kuanza kunifwata kwa mendo wa taratibu kuja sehemu nilipo.Nikataka kurudi nyuma ila nikijikuta miguu inazidi kuwa mizito na kubaki nikiwa nimesimama kama mlingoti.Likanisogelea na kuushika mkono wangu wa kulia,akautazama sehemu ya giganja na gafla sehemu ya juu ya kiganja,akaing’ata na kuanza kuinyonya damu.

Kitu kilicho nishangaza,sikuweza kupata maumivu ya aina yoyote japo ninaona damu zinanichuruzika pembeni.Kitu kilicho zidi kunishangaza,kila jinsi anavyozidi kunyonya damu yangu ndivyo jinsi anavyo badilika.kutoka katika uzee kurudi kwenye ukijana zaidi.Akaniachia mkono wangu na kuwa kijana mdogo kama wa umri wa miaka kumi na mbili huku akifanana na mimi kila kitu ambacho mimi ninacho,kuanzia sura
“Nikinyonya zaidi,damu yako nitarudi kuwa mtoto”
Alizungumza na kuzidi kunishangaza.Akanitazama kwa macho makali kisha akarudi na kukaa kitandani,akachukua shuka na kujifunga
“Baba njoo ukae hapa”
Alinionyesha sehemu ya kukaa,pembeni ya kitanda,taratibu nikajizoa zoa hadi kitandani na kukaa pembeni yake.Ukimya wa dakika kadhaa ukakatiza wakati wote nikiwa nikimtazama jinsi alivyo

“Baba,ninaamini kuwa mutakuwa munaniona kuwa mimi ni kiumbe cha ajabu sana kutokea kwenye maisha yanu”
“Hapaana,mwanangu”
Nilijikaza tuu kusema hiyo mwanangu ila kiukweli,sina imani naye kabisa huyu mtoto ambaye kwa sasa ninafanana naye na wala siwezi kupinga kitu cha aina yoyote.
“Baba mimi ni binadamu ila pia ni shetani”
Nikastuska kidogo,japo nimepewa mamlaka yakuwaongoaza viumbe wa aina hii,ila kwa hapa mapigo ya moyo yakapoteza kabisa muelekeo wake
“Usistuke,baba.Kwa jina munaweza kuniita Lusifah”
Kwa mara ya kwanza maishani mwangu kuona mtoto anajichagulia jina la kujiita tena jina lenyewe ni lakishetani.
“Kwa nini nikuite hivyo?”
“Ndilo jina ambalo mimi nimepewa kabla ya kuzaliwa”
“Kabla ya kuzaliwa kivipi?”

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )