Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 12, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Nane ( 28 )

adv1
AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Gafla nikahisi kitu kiki nikuvutwa mguu kwa nyuma na nikageuza sura yangu nyuma kwa haraka kuangalia ni nini kilicho nigusa sikuona kitu cha aina yoyote na kujikuta nikitumia nguvu kujivuta mbele na kitu hicho kikaniachia na kustukia nikipoteza muhimili wa mwili wangu na kujikuta nikilala kwenye sehemu laini(signboard) ya juu kwenye chumba changu ambayo haiwezi kuhimili uzito wa mwili wangu na kujikuta nikipitiliza moja kwa moja na kuanguka chini ndani ya chumba changu na kutoa kishondo kizito

ENDELEA
Kufumba na kufumbua sikuona mtu yoyote ndani ya chumba changu zaidi ya Rahma aliye lala kitandani akiwa hajitambui na nikasikia kelele na vishindo vya wanandugu wa Rahma sebleni kila mmoja akijaribu kuokoa maisha yake nikajua kwamba hawakutarajia kuuona uwepo wangu ndani ya chumba changu tena kwa mfumo huu wa kuanguka kutoka darini.Nikanyanyuka japo sehemu ya mbavu za kushoto ninahisi maumivu makali ila nikajikaza na kuchungulia mlangoni  sikuona mtu yoyote akitokea sebleni.Kwa haraka nikaingia jikoni kwangu na kuchukua kifuko cha unga wa ngano na kujimwagia unga wote mwilini mwangu na nikausambaza vizuri usoni mwangu.Nikachungulia sebleni nikaona vivuli vya watu wawili wakiwa wanakaribia kuingia ndani huku wakinyata wakitaka kuchungulia ni nini kilicho tokea

“Let’s go”(twendee)
Nilijisemea kwa sauti ya chini na kuchomoka kwa kasi jikoni huku nikitoa mlio wa pikipiki aina ya XL Baja na kuwafanya watu waliokuwa wakinyata mlangoni kukurupuka na kuanza kukimbia kurudi walipo tokea huku baba Rahma nikimpiga kikumbo getini na kumbwaga chini na kuwafanya wamama walio simama nje baada ya kuniona wakatawanyika kwa woga na kila mmoja akashika njia yake na kusababisha nao pia kuapiga kelele.

Breki ya kwanza nikasimama ndani ya maji kwenye fukwe almaarufu kwa jina la JET na sikujali watu wamenichukuliaje.Japo kuwa siwezi kuogelea vizuri ila ikanibidi nipate ujuzi wa kupiga mbizi na kwenda mbali kidogo na ufukwe ulipo na nikakaa ndani ya maji huku nikiwa nimekiacha kichwa nje kwa ajili ya kuvuta punzi zaidi ya masaa manne hadi giza likatanda angani ndipo nikatoka ndani ya maji
Sikuwa na hamu ya kwenda nyumbini kwangu kwa maana nikahisi ni lazima watakuwa wananitafuta kwa udi na uvumba.Nikapiga mwendo hadi nyumbani kwa madam Zena huku nguo zangu zikiwa zimelowa.Nikagonga mlango kwa bahati nzuri akafungua madam Zena akiwa amevalia suruali na tisheti kubwa na akaonekana kunishangaa baada ya kuniona

“Ehhee Sir Eddy vipi mbona umelowaa?”
“Shosti wee acha tuu hembu twende tukayazungumzie ndani la sivyo yaliyo nikuta huko yasije yakanikuta na hapa”
“Ehee Eddy leo umeniita shosti......Haaahaaa kweli huko ulipo toka umevurugwa”
“Tena sijavurugwa kidogo...Nimevurugwa sana”
“Haya yaliyo kukuta ni yapi Shost yangu?”
Sikuwa na sababu ya kumficha madam Zena kwa maana endapo nikimficha ipo siku mambo yanaweza yakaniharibikia na akashindwa kunisaidia kabisa.Hadi na maliza kumsimulia Madam Zena akawa anacheka hadi machozi yanamtoka na kujikuta amekaa chini akiendelea kucheka
“E.....Eddy hapo kama ninakuona vile na hayo maunga yako”
“Wee nilikodi pikipiki ya Baja...yaani niliondoka na gia tatu badala ya moja au mbili na kwajinsi nilivyokuwa ninatisha hapakuwa na mganga wala hapakuwa na baba wa mtoto wote changu na mimi kiulaini nikasepe”
“Hii kali ya mwaka Eddy”
“Wee acha tuu najuta kuja Tanga?”
“Kwa nini?”

 
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )