Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 1, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Nane ( 18 )

adv1
AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA Nikakata simu na kuendelea na safari yangu na kwa mbali kutoka nilipo hadi ilipo nyumba ya bibi nikaona nje kumefungwa turubai huku watu walio valia kanzu wakiwa wamekaa kwenye majamvi huku ukimya ukiwa umetawala katika endeo hilo.Nikazidi kuongeza mwendo huku akilini wazo la bibi kuwa amefariki dunia likaanza kunitesa,Kabla sijafika karibu na sehemu ilipo nyumba ya bibi nikastuka mtu akinishika mkonno kwa nyuma huku akinivuta kwa nguvu

ENDELEA
     Nikageuka na kukutana na sura yam zee wa makamo akiwa amavalia kanzu nyeupe na barakashea huku mkononi mwake akiwa ameshika mkongojo wa kumsiadia katika kutembelea
“Shikamoo mzee”
“Shikamoo yako haina msaada wowote kwangu”
Mzee alizungumza kwa hasira huku akiachia msunyo mkali hadi nikabaki ninamshangaa huku nikijiuliza nilicho mkosea ni nini
“Wewe kijana ni mbaya sana…..Kijana huna adabu shiii nkumi,kijana huna busara.Yaani umeona haitoshi umeamua kutuma majini yako kuja kumdhuru mke wangu”
“Mzee mbona sikuelewe umechanganyikiwa nini?”
“Mimi nimechanganyikiwa.PUMBAVU SANA WEWE”
Mzee akanichapa bakora moja na kunifanya nimponyoke mkononi mwake na kusimama pembeni nikiwa ninamshanga huku watu wengine walio karibu yetu wakitushangaa kwa tukio alilo lifanyia babu

“Vijana wa siku hizi hamuuna adabu sana unaniambia nimechanganyikiwa mimi?”
“Oya brother Eddy huyo mzee ni kichaa asikupotezee muda wako wewe achana naye”
   Alipita jamaa mmoja na kuniambia kuhusiana na huyo mzee ambaye kwenye macho yangu sikuwahi kumuona siku hata moja katika mtaa nilio kuwa nimekaa.Nikaamini mzee hana akili vizuri baada ya kuanza kumkimbiza kijana aliye niambia kuwa mzee huyo ni kichaa.Nikajiweka vizuri shati langu na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya bibi iliyo jaa watu nje wenye kanzu nyeupe.Bibi akaniona na kuja kunifwata na kunikaribisha na kunionyesha stuli isiyo kaliwa na mtunkisha nikaichukua na tukasogea kidogo na kukaa pembeni na walipo watu wenye kanzu nyeupe huku bibi akikaa juu ya gogo la muembe ulio katwa siku nyingi
“Bibihapa kuna nini?”
“Ni maulidi ya mwanangu mmoja wa kike anayafanya kwa mtoto wake alieye zaliwa miezi kadhaa ya nyuma”

“Ahaaa mbona kumetulia sana?”
“Ahha ndio wanamalizia malizia…”
“Inamaana watu tayari wameshamaliza kula ubwabwa?”
“Ubwabwa wamekula tangua amchana hapa wanasubiri kufunga maulidi”
“Bibi bwana mimi nimekuja nina tatizo tena sio dogo nitatizo kubwa kiasi kwamba ninajikuta nimechoka kwenye tatizo lenyewe”
Bibi akaanza kucheka na kwajinsi ya meno yake kuwa pungufu mdomoni mwake na kuweka mapengo makubwa ikanilazimu na mimi kuanza kumcheka
“Eddy mjukuu wangu ile jana ulivyo kuwa unahama unakumbuka nilikupa nini?”
“Ulinipa maji kwenye kichupa?”
“Uliyatumia?”
“Bibi nisikudanganye nilisahau?”
“Hapo ndipo ulipo kosea na yule msichana uliye hama naye ndio aliye kusababishia matatizo hayo”
“Amenisababishia matatizo hayo kivipi?”
“Ngoja nikuambie kitu usicho kijua kuhusu yule msichana”
Nikajiweka vizuri kwanye stuli niliyo ikalia huku nikimtazama bibi kwa umakini 

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )