Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, March 16, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Mbili ( 32 )

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

“ILA BABA KWANINI UMUUE EDDY WANGU?”
Swali la Rahma likawafanya watu wote kumtazama na nikaanza kuziona sura za askari zikianza kubadilika na kuweka mikunjo askari wawili wakaziweka bunduki zao sawa kuzielekeza kwa baba Rahma  huku mkuu wao akipiga hatua hadi kitandani na kumuuliza Rahma swali
“Unasema kuwa Eddy ameuliwa na baba yako?”
‘NDIO”

ENDELEA
Chumba kizima kikatawaliwa kwa ukimya kiasi kwamba kila mmoja macho yake yakamgeukia baba Rahma
“Huyo Eddy kwako alikuwa ni nani?”
“Ni mpenzi wangu ninaye mpenda sana”
Nikanyata taratibu huku shangazi Rahma akiwa anaendelea kuwaomba askari waweze kuzungumza juu ya swala alilo lizungumza.Nikashuka kwenye ngazi za gorofa lao na nikatoka nje na moa kwa moja nikeelekea nje na safari ya nyumbani kwangu ikaanza.Moyoni mwangu nikaanza kuhisi hizto na wa ushindi mkubwa kwani swala la kuingia nyumbani kwa kina Rahma pasipo wazazi wake kufahamu na nimtu mmoja ndio amelitamvua hilo kidogo likanipa faraja ya kuweza kumtorosha,nikanawa sura yangu na nikarudi katikahali yangu ya kawaida

Siku nzima nikajifungia ndani na sikutoka nje huku nikiwa ninapanga mipango ya kumtorosha Rahma katika hali ya kawadi,Picha nyingi nilizo zichora kwenye karatasi nyeupe zikiwa kama ramani ya nyumba ya baa Rahma zinakanitosha zaidi kujua kuwa ninaanzia wapi katika kufanikisha swala la kumtorosha Rahma hadi nikajikuta ninapitiwa na usingizi katika kocho nililo kalia.Asubuhi na mapema nikaelekea nyumba ya pili kwa mzee mmoja ambaye na mstaafu wa jeshi na kipindi cha nyuma aliniomba niweze kumfundisha mwanaye wa kiume masomo ya kumbo yake ya PCM na kwa bahati mbaya sikuweza kupata muda huo kutokana na matatizo
Nikagonga geti lake nalikafunguliwa na mlinzi na akaniruhusu kuingia ndani na kwabahati nzuri nikakutana na mzee Ngoda akifanya mazoezi kwenye moja ya bustani yake na nikamfwata hadi sehemu alipo na kumsalimia
“Vipi Eddy kuna siku nilisikia sikia kelele huko kwako ila kutokana nilikuwa ninawageni muhimu sana nikashindwa kutoka”
“Mzee wee acha tuu kuna mambo mengi yalinikumba hivi vijiwiki kadhaa vya nyuma nikajikuta hata ninashindwa kutimiza ile ahadi ya kumfundisha mwano”

“Mambo gani kwa maana nilipo kuja kuchungulia sikukuta mmtu zaidi ya ukimya mwingi?”
Nikaanza kumsimulia mzee Ngoda kuanzia mwanzo hadi mwishio kuhusiana na mkasa wa Rahma hadi ninamaliza akabaki akisikitika huku akishusha pumzi nyingi mara kwa mara
“Duuu sasa wewe unataka nikusaidie nini juu ya hilo swal lako?”
“Mimi ninataka unisaidie juu ya mipango na mbinu za kijeshi ili niweze kwenda kumtorosha yule binti”
“Hjui hilo ni kosa la jinai na kama ukikamatwa hapo unachukuliwa kuwa kama gaidi na kifungo chake nina imani unakijua”
“Ndio ninakutambua mzee wangu ila naomba tuu unisaidie”
“Wee koma wenyewe wanasema uzee mwisho msata kila mtu mjini ni baby”
Nikajikuta nikangua kicheko kwani sikutegemea kama mzee ataweza kuniropokea maneno ya namna hii ukilinganisha na umri wake.

“Eddy mimi kama mimi kwenye hilo sinto weza kukusaidia labda kuna jengine useme nitakusaidia kwa maana nitakuwa nimevunja sheria na kanuni za jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na sheria za jeshi.”
Mzee Ngoda akanikatalia kata kata na sikuwa na kingine cha kuzungumza zaidi ya kuondoka zangu na kurudi nyumbani kwangu.Nikajipikia kifungua kinywa na baada ya kumaliza kupata chai nikaelekea kwenye maduka ya wachaga yaliyopo barabara za namba na kazi yangu ikawa ni kutafuta ni nguo gani ninaweza kuzinunua na kuzivaa na zikabadilisha muonekano wangu kabisa.Hadi mwisho wa mizunguko yangu nikajikuta nikinunua overol jeusi pamoja na kofia kubwa na kurudi nyumani kwangu mida ya saa kumi na moja jioni.Nikapanda kitandani na kulala huku saa yangu ya mkononi niiitega muito wa kunistua saa nne usiku.

Kama nilivyo itega saa yangu ndivyo ilivyo niamsha nikanyanyuka kitandani na kuingia bafuni na kunawa uso ili kutoa uchovu kisha nikarudi  ndani na kuvaa overoli langu na pamoja na kofia,Nikatafuta mabuti yangu ya mvua kisha nikavaa,nikazichukua karatasi nilizo chora ramani ya nyumba ya kina Rahma na kuanza kuipitia moja baada ya nyingine.Nikachukua beki langu dogo na lenye vijimikanda vyembaba na kulivaa mgongoni huku likiwa ni vifaa kama koleo,bisibisi na nyundo

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )