Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, April 16, 2018

Ikulu: Hatuna Taarifa na Tuzo ya Rais Magufuli Kutoka Ghana

Mkurugenzi  wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa amesema Ikulu haina taarifa kuhusu tuzo aliyoshinda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia, Dkt. John Magufuli nchini Ghana, kama Kiongozi Bora Barani Afrika.

Msigwa ameeleza kwamba, inafahamika utaratibu wa tuzo yoyote lazima mtu anayetunukiwa apewe taarifa rasmi, lakini mpaka sasa hawajapokea taarifa yoyote kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo, hivyo hawajui lolote kama ni kweli au la!

“Hatuna taarifa ya tuzo hiyo, tunavyojua ni kwamba mtu yeyote anayetunukiwa tuzo lazima apewe taarifa rasmi kutoka kwa watoaji, sasa hatujapata taarifa yoyote mpaka sasa, nasikia ndio tuzo ambazo kina Monalisa wameshinda, lakini hatujapokea taarifa rasmi kuhusu tuzo hiyo, hivyo siwezi nikaizungumzia”, amesema Msigwa.

Tuzo hiyo ambayo imetajwa kuwa ameshinda Rais Magufuli, imetolewa jana Jumapili, Aprili 15, 2018 jijini Accra, Ghana, ambapo pia Watanzania wengine katika tasnia ya filamu waliibuka washindi akiwemo Yvone Chery ‘Monalisa’ na Vincent Kigosi ‘Ray’.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )