Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, April 14, 2018

Kilichomfanya mbunge akapiga magoti bungeni

Mbunge wa Ileje (CCM) Janeth Mbene amepiga magoti bungeni na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kupeleka maendeleo kwenye wilaya yake anayodai ilisahaulika.

Mbene amefanya kitendo hicho jana bungeni Aprili 13, wakati akichangia bajeti ya ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Mara baada ya kuruhusiwa kuchangia bajeti hiyo, Mbene alisema wilaya ya Ileje ni ya miaka mingi lakini ilikuwa haina barabara ya lami lakini katika Serikali Awamu ya Tano, barabara imejengwa.

Katika kuonyesha kuwa jambo hilo limemfurahisha, mbunge huyo alipiga magoti, pembeni ya kiti anachoketi bungeni akimshukuru Rais Magufuli.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )