Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, April 12, 2018

Mmiliki Wa Mabasi Ya HBS Na Sabena Ajiua Kwa Kujipiga Risasi

Mmiliki wa kampuni mbili za mabasi za HBS Express na Sabena, Sultan Ahmed maarufu kama Chapa, amejiua kwa kujipiga risasi mdomoni iliyotokea kisogoni nyumbani kwake Sikonge mkoani Tabora jana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wilbrod Mutafungwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana mkoani humo.

Kamanda Mutafungwa alisema tukio hilo lilitokea jana saa 2:30 asubuhi nyumbani kwa marehemu na kwamba chanzo cha kujiua kwake huko hakijafahamika.

"Bado tunachunguza tukio hili, amejipiga risasi mdomoni, tunachunguza chanzo cha tukio hili," alisema Kamanda Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa alisema marehemu Chapa pia alikuwa akimiliki kituo cha mafuta ya petroli wilayani Sikonge.

Chapa anakuwa mfanyabiashara wa pili nchini kujiua kwa kujipiga risasi katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya Festo Msalia, muuza vinywaji kwa bei ya jumla mkoani Dodoma, kujilipua Machi mwaka jana.

Msalia alijiua kwa kujipiga risasi kichwani baada ya kukamatwa na shehena kubwa ya viroba.

Aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoani humo wakati huo, Lazaro Mambosasa alisema marehemu aliondoka nyumbani kwake kwa kutumia gari aina ya Toyota Prado na kwenda kujipiga risasi katika eneo la Veyula, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Mfanyabiashara hiyo alikamatwa na shehena ya viroba Machi 3, mwaka jana.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )