Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, April 19, 2018

Nuh Mziwanda Amtaka Diamond Aache Kudhalilisha Wanawake

adv1
Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amemjia juu msanii mwenzake Diamond Platnumz na kumtaka aache vitendo vyake anavyofanya vinavyopelekea kudhalilisha wanawake.

Nuh ameongelea kitendo cha Diamond kusabaza video Kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wanawake wawili tofauti katika usiku mmoja kama udhalilishaji wa wanawake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Nuh Mziwanda amedai kitendo alichokifanya Diamond sio cha kiungwana kwani wanawake wote ni kama mama zetu hivyo tunapaswa kuwaheshimu.

"Ni lazima tuwaheshimu wanawake maana ndio waliotuzaa na waliotuleta duniani kwahiyo automatically ni watu wa kuwaheshimu na hiyo ni nguvu ambayo Mwenyezi Mungu kaiweka ......kwaiyo huwezi ukarekodi vitu kama vile alafu ukaviweka Kwenye mitandao inakuwa inaleta picha mbaya kama vile dada zetu hawana thamani kitu ambacho sio cha kweli”.

Tangu kitendo hiko kitokee siku chache zilizopita tayari Diamond ameshachukuliwa hatua za kisheria na Waziri Mwakyembe  amehaidi atafikishwa mahakamani
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )