Sunday, April 22, 2018

Polepole: CCM Haijamkosoa CAG......CHADEMA Ndo Waliomkosoa

Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya CCM, Humphrey PolePole amefunguka na kusema kuwa wao kama Chama Cha Mapinduzi na serikali hakuna mtu kati yao aliyemjibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad bali CHADEMA ndiyo wamemjibu.

Polepole amesema hayo leo April 22, 2018 kupitia mtandao wake wa twitter na kudai kuwa wao waliipokea ripoti hiyo na kumpongeza CAG na kuitaka serikali iendelee kuchukua hatua katika yale ambayo CAG ameyabaini.

"Kimsingi kwa CCM au Serikali yake hakuna hata mtu mmoja ambaye amemjibu CAG, sisi tulipokea, tulipongeza na tukaelekeza Serikali iendelee kuchukua hatua. Ambaye amejitokeza kujibu hadharani ni CHADEMA ndio pekee wamemjibu na kumkosoa CAG. Ila naona watu wachache pamba masikioni" alisisitiza Polepole

Polepole anasema yeye alipowaita waandishi wa habari hakumjibu CAG bali amedai kuwa alifanya ufafanuzi wa hoja mbalimbali ikiwepo ile ya Trilioni 1.5 ambayo kwenye ruipoti ya CAG inaonekana haina maelezo.

"Kuna tofauti kati ya kumjibu CAG na kufafanua hoja ambazo amezitoa kwa CCM na kuulaani vikali upotoshaji wa Zitto Kabwe juu ya taarifa ya CAG" 

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )