Wednesday, April 18, 2018

Serikali yawasimamisha kazi mawakili sita

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema mawakili sita wamesimamishwa kufanya kazi ya uwakili kwa miezi sita hadi miaka mitano kwa makosa ya nidhamu.

Kabudi ameyasema hayo leo bungeni wakati akiwasilisha mipango wa makadirio ya bajeti ya wizara ya Katiba na Sheria.

Amesema uamuzi huo umetolewa na kamati ya nidhamu ya mawakili baada ya kupokea malalamiko hayo

Profesa Kabudi, amesema kamati hiyo ilipokea malalamiko 18 ya mawakili kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na hivyo kufanya jumla  ya malalamiko yaliyokuwa mbele ya kamati kufikia 48.

“Katika kipindi hicho, malalamiko 22 yalisikilizwa na kutolewa uamuzi ambako mawakili sita wamesimamishwa kazi ya kufanya uwakili kwa muda wa miezi sita hadi miaka mitano,” amesema.

Ametoa wito kwa mawakili wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu wakitambua kuwa wao ni maofisa wenye dhamana kubwa ya kufanikisha utoaji wa haki kwa wakati.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )