Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, April 4, 2018

Taarifa rasmi kutoka Vodacom kuhusu upatikanaji wa huduma ya LUKU

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc inapenda kuwataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kwamba, itaendelea kutoa huduma ya ununuzi wa umeme (LUKU) kupitia mfumo wa malipo wa serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG).

Kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa hivi karibuni na kampuni ya kuzalisha na kutoa huduma ya umeme nchini (TANESCO) kuhusu kuanza kutoa huduma ya kununua umeme kwa kupitia mfumo wa Serikali wa GePG, Vodacom Tanzania Plc inapenda kuwatoa hofu Wateja wake kwamba wataendela kupata huduma ya kununua umeme ya LUKU kupitia Vodacom M-Pesa kama ilivyokuwa mwanzo.

Mfumo mpya utaiwezesha Tanesco kuunganisha mauzo moja kwa moja kutoka makampuni mengine ya simu na mabenki kwenda GePG ikiwa ni matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.

Kutakuwa na ongezeko la asilimia moja nukta moja ya gharama halisi (1.1%) anayotozwa mteja ili kununua umeme pindi atumiapo huduma ya M-Pesa.

Vodacom inawahakikishia Wateja wake kwamba itaendelea kutoa huduma ya LUKU kupitia M-Pesa ambayo pia inapatikana katika App za Apple, na Android.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )