Tuesday, April 17, 2018

TAKUKURU Kuwafikisha Mahakamani Viongozi Waliotafuna Bilioni 2

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iko katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Bilioni mbili zinazowakabili viongozi wa kiwanda cha kukoboa Kahawa cha mkoani Kilimanjaro.

Viongozi kadhaa wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Vyama vya Ushirika katika Kanda ya Kaskazini wanatuhumiwa kuuza nyumba za ushirika kisha kununua mtambo feki wa kukoboa Kahawa ambao haujafanya kazi tangu ununuliwe miaka minne sasa.

Kaimu Kamanda wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro, Moses Oguda amewaambia waandishi wa habari kuwa baadhi ya majalada ya kesi hiyo yamerejeshwa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kwa ajili ya utekelezaji.

TAKUKURU pia imepokea taarifa za rushwa zipatazo kumi na tano na kuzifanyia kazi, nyingi kati ya hizo zikiwa ni kutoka idara za Elimu, serikali za mitaa, polisi na Mahakama.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )