Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, April 14, 2018

Vodacom M-pesa Yapewa Tuzo Na Kutambuliwa Na Gsma Kwa Huduma Zilizotukuka


Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya M-PESA imetambuliwa nakupatiwa cheti kutambua ubora uliotukuka wahuduma za kifedha. 


Tuzo hii imetolewa jana jijini Abidjan, Côte d’Ivoire kutambua usalama na uhakika pamoja na nia thabiti ya M-Pesa katika kulinda haki ya mteja.

Tuzo hii imetolewa bada ya Vodacom Mpesa kufiika vigezo vilivyowekwa na GSMA ambavyo ni viwango vya juu vya kulinda amana ya mteja, usalama wa huduma, usiri na kulinda taarifa za mteja, kupambana na utakatishaji fedha, kupambana na wanaogharamia vikundi vya ugaidi, na pia kupambana na mbinu zote za udanganyifu.


Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaj iwa Vodacom anasema“Utambuzi na cheti hiki vinathibitisha nia na utendaji wa Vodacom Tanzania katika kuhudumia na kulinda haki za mteja katika eneo lote la biashara ya MPesa, tukiwa ni mtandao unaoongoza kwa huduma ya pesa cheti hiki kitatupatia nafasi ya kuaminika zaidi nakutuongezea ari yakiutendaji ili kuwaridhisha wateja wetu ambao  wametufanya kuwa kampuni ya simu ya kwanza nchini kupata utambulisho huu baada ya kufikia vigezo," alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom.
 

Chetihiki cha GSMA kimekuja wakati ambapo Vodacom Mpesa inatimiza miaka 10 ya M-pesa Tanzania.

Kwa takribani miaka 10 sasa M-pesa imeweza kubadilisha maisha nakuipandisha Tanzania kiuchumi kupitia huduma za kutuma na kutoa fedha,malipo ya  bili,akaunti za kutunza fedha,mikopo na mengineyo mengi.

M-pesa leo ina zaidi ya wateja milioni 8,wakala 106,000,biashara za kawaida zaidi ya 2000,wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 15,000,benki zilizounganishwa zaidi ya 30.

Kupitiahudumazake M-pesa imewezesha wakazi wakitanzania wa mijini na vijijini kuwa sehemu ya mfumo mzima wakiuchumi unaotambulika,pamoja na ongezeko kubwa la kiuchumi katika jamii nyingi za kitanzania.

Mfumo huu rasm inchini Tanzania umekuza uchumi kwa mwaka 2017 hadi kufikia 65% kutokea 58% mwaka 2013 na 44% kwa mwaka 2009 Mwaka mmoja baada ya M-pesa kufunguliwa rasmi nchini Tanzania.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )