Wednesday, April 4, 2018

Wafuasi 27 Wa Chadema Washikiliwa Na Polisi kwa Kufanya Vurugu Mahakamani

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu 27 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema kwa tuhuma za kufanya fujo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiendelea mahakamani hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa wanaoshikiliwa ni wanaume 20 na wanawake saba, ambao walikamatwa katika eneo la Mahakama hiyo wakifanya fujo wakati wakisubiri uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya hatima ya dhamana viongozi hao saba wa Chadema.

“Watu hao walikuwa wanafanya vurugu katika eneo la Mahakama wakati Mahakama inaendelea, tumewashikilia na tutawafikisha mahakamani tukikamilisha taratibu,” alisema Mambosasa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )