Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, May 7, 2018

Bulaya ataka Wabunge, Mawaziri wakatiwe maji

Mbunge wa Bunda Mjini ( CHADEMA ), Ester Bulaya amesema tatizo la maji ni kubwa nchini, akipendekeza mawaziri na wabunge kukatiwa huduma hiyo ili waone adha wanayoipata wananchi.

Mbunge huyo ameyasema hayo leo Mei 7, 2018 alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya mwaka 2018/19, ambapo ameweka wazi kwamba  fedha zinazotengwa huwa hazitolewi.

Mbunge huyo amesema wabunge na mawaziri wakikatiwa maji watahisi uchungu wanaopata wananchi wa kukosa maji safi na salama kwani kuna hospitali zinashindwa kufanya upasuaji kwa kukosa maji, huku wanawake wakipata adha.

Mbunge huyo ameenda mbali na kuongeza kwamba hali ilivyo sasa ni bora mgonjwa akapelekewa ndoo ya maji kuliko chakula.

Mbali na hayo Mbunge huyo ameongeza kwamba hata vijana wanapohamasishwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji kama hakuna maji ni kazi bure.

“Tunaguswa na tatizo la Watanzania, tunaguswa na tatizo la ajira kwa vijana, ambao wanakwenda kuwekeza katika kilimo lakini hakuna maji,” amesema
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )