Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, May 2, 2018

Familia ya kina Heche yaukataa msaada Uliotolewa na Polisi

Siku chache baada ya mkazi wa Tarime, Suguta Chacha kufariki dunia akiwa mikononi mwa polisi, familia yake imekataa kupokea msaada wa chakula kilichotolewa na ofisi ya kamanda wa polisi, Kanda Malumu ya Tarime/Rorya.

Chakula hicho kilitolewa na jeshi hilo kwa ajili ya shughuli za msiba wa Suguta ambaye ni ndugu wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche aliyefariki Aprili 27 akiwa mikononi mwa polisi.

Msaada huo wa kilo 100 za mchele, unga kilo 100, maji ya kunywa katoni 20 pamoja na sukari uliwasilishwa msibani hapo  na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Henry Mwaibambe lakini ulikataliwa.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo Kamanda Mwaibambe alisema: “Tuliache kwa sababu halina maana tena na tunapenda liishe salama.”

Katibu wa ukoo wa Suguta, Chacha Heche alisema familia hiyo iko tayari kupokea msaada wa Kamanda Mwaibambe kama mtu binafsi kutokana na jinsi alivyoshirikiana nao tangu mauaji hayo yatokee, lakini haitapokea msaada wa polisi kama taasisi.

“Tutapokea msaada kutoka kwa yeyote mwenye mapenzi mema lakini siyo taasisi ya Jeshi la Polisi. Tayari tumechanga zaidi ya Sh5 milioni kati ya Sh8 milioni zinazohitajika kugharamia mazishi ya ndugu yetu,” alisema Heche.

Alisema familia inaheshimu na kutambua jinsi Kamanda Mwaibambe anavyoshughulikia tukio hilo na itashirikiana naye na kumkaribisha katika mazishi kama mtu binafsi na siyo kwa kofia ya polisi.

Katibu huyo wa ukoo wa Suguta, alisema marehemu atazikwa kesho baada ya ndugu kujiridhisha na hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi.

Suguta anadaiwa kufariki dunia baada ya kuchomwa visu na askari polisi, William Marwa (50).

Marwa alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime juzi na kusomewa shtaka la mauaji.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mwani Mrisho alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 27 ambako alimuua Suguta (27) kwa kumchoma na kisu.

Tukio hilo lilitokea usiku wa siku hiyo baada ya Suguta na mmiliki wa baa kukamatwa na polisi waliokuwa doria. Hata hivyo, ndugu wa Suguta walipokwenda kumuangalia siku inayofuata waliambiwa amefariki na mwili upo mochwari.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )