Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, May 4, 2018

Mama Kanumba Apata Mualiko Nchini Burundi

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Bi. Flora Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba Amelamba shavu zito baada ya kupata mualiko wa kuenda nchini Burundi.

Mama Kanumba Amepata mualiko maalumu kutoka kwa wasanii wa filamu wa nchini Burundi kwa ajili ya kuenda kujifunza kazi za sanaa hasa filamu wanazofanya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Mama Kanumba alisema kuwa baada ya kupata mualiko huo kutokana na wasanii hao kuthamini mchango wa marehemu mwanaye, ameona ni vyema kwenda na kitu nchini humo ambapo ataizindua filamu yake inayoitwa Capten Habona.

"Yani najisikia ni mtu ambaye ninaheshimika ingawa mtoto wangu hayupo hivyo filamu yangu hiyo nitazindulia huko kwa vile na wao wamenipa heshima kubwa sana kwa kuwa filamu yenyewe ina historia nzuri sana“.

Mama Kanumba aliingia Kwenye sanaa miaka michache iliyopita mara baada ya Steven Kanumba kufariki dunia ambapo alikiri sababu za kimaslahi ndizo zilizomuingiza Kwenye uigizaji japokuwa mwanaye hakupenda aigize.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )