Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, May 9, 2018

Mbunge CHADEMA Ahoji MAFISADI Kuhamishwa Vituo vya Kazi Badala ya Kutumbuliwa

Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema) Esther Matiko amesema Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa watendaji ambao miradi wanayoisimamia imegubikwa na ufisadi na badala yake imekuwa ikiwahamishia maeneo mengine.

Akichangia katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka 2018/19, Matiko amesema kuwa kuna mradi wa Geita ambao ulitumia Sh 6.6 bilioni lakini umeshindwa kutoa maji.

“Ufisadi umekithiri katika miradi ya maji nchini hata hizo fedha kidogo zinazoenda katika miradi ya maji bado zinaliwa. Serikali imekuwa ikisema inapambana na ufisadi lakini hatuoni hatua zikichukuliwa kwa wanaokula fedha za miradi ya maji matokeo yake huyu mtendaji wa Geita mlimchukua mkamhamishia wizarani,”amesema.

Amesema anaungana na wabunge wenzake waliotaka kuundwa kwa kamati ya Bunge ya kuchunguza miradi ya maji kama ilivyokuwa katika maeneo mengine yaliyowahi kuchunguzwa na kamati za Bunge.

“Asilimia tano ya watu ndio wanatumia ndege. Hivi kipaumbele ni ndege ama maji ambayo yanatumiwa na watu asilimia 100?”Amehoji.

Amesema maji ni uchumi, kwamba viwanda haviwezi kujengwa bila kuwa na maji, “ukiwezesha Watanzania kuwa na maji, mambo mengine yatafanikiwa yenyewe.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )