Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, May 3, 2018

Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga Alitaka Jeshi la Polisi Kutumia Nguvu

Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kutumia nguvu alizonazo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatukana viongozi.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa 2018/19, Mlinga amesema;

“Matusi mitandaoni ni 'too much', kwenye mitandao hajulikani Rais ni nani, kiongozi ni nani, kuna akaunti nyingi zinatukana, wanatukanwa wananchi, mawaziri mpaka Rais. IGP uko hapa tumekuwekea hizo nyota mabegani ni nguvu, tumia nguvu zako wasikuchezee. Mfano natoa akaunti zinazomtukana rais ni kama Kwinyara, Malisa GJ, Yericko Nyerere na Dada yao Mange Kimambi wamekuwa wakimtukana rais". 

Mlinga licha ya kupongeza utendaji wa polisi, amedai asilimia 85 ya huduma inayotolewa na jeshi hilo inahusisha rushwa ingawa anasema askari wa kike hawamo kwenye kundi hilo.

“Kesi ya kuku inakuwa ya ng’ombe, kesi ya kutusi inakuwa ya kuua kwa maneno, lakini niwapongeze wanawake katika hili hawamo,” amesema Mlinga huku akishangiliwa.

Amesema matukio ya kamatakamata yanayofanywa na Trafiki: “Ni janga la Taifa, wanaitwa wana mapato Dar es Salaam huko wanaitwa Tigo. Bodaboda ndiyo kabisa usiseme, ukienda katika vituo vya polisi, pikipiki ni nyingi.”

Naye mbunge wa Mlimba (Chadema), Susan Kiwanga amesema; “Kazi ya polisi si kunipangia cha kusema katika mkutano. Kama unaona nakosea subiri niongee nikimaliza  ukiona nimekosea nikamate.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )