Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, May 18, 2018

Mgombea CCM Akamatwa Akigawa Rushwa

Mgombea wa nafasi ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kilangala, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Jenga Mohamedi  na wajumbe saba wa Mkutano Mkuu wa kata wa chama hicho wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakidaiwa kupokea na kutoa rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 18, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Steven Chami amesema watu nane wamekamatwa akiwamo Mgombea ukatibu aliyekutwa akitoa rushwa kwa wajumbe ili achaguliwe.

Kwa mujibu wa Chami, tukio hilo limetokea jana saa mbili asubuhi kwenye eneo la uchaguzi huku watuhumiwa wakiwa  na fedha Sh 2,000  kila mmoja huku mpambe wa mgombea huyo alikutwa na bulungutu kiasi hicho cha fedha zenye thamani ya Sh 50,000 na orodha ya majina ya wajumbe wa mkutano huo.

Alisema watuhumiwa wanashikiliwa  na Taasisi hiyo hadi mahojiano yatakapo kamilika na hatua zingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )