Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, May 21, 2018

Waziri Mkuu kuzindua miradi mikubwa mitatu leo Lindi

adv1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kutua mkoani Lindi leo ambapo atazindua mradi wa kuunganisha mkoa huo na wa Mtwara katika gridi ya Taifa.

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa jana Mei 20 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Waziri Mkuu.

Alisema kwa siku ya leo, Waziri Mkuu atazindua miradi mikubwa mitatu ukiwamo wa kuunganisha Lindi na Mtwara kwenye gridi ya taifa.

Pia Waziri Majaliwa atakagua miundombinu ya uingizaji mafuta katika mkoa huo ambao unatarajia kuanza kupokea mafuta ya petrol na dizeli mwezi ujao.

“Atakwenda kujionea miundombinu ya uingizaji mafuta kupitia bandari ya Mtwara, habari njema iliyopo kuanzia Juni utaanza kupokea mafuta kupitia bandari ya Mtwara,” alisema Byakanwa.

Alisema Waziri Mkuu atakwenda kwenye uzinduzi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme Mtwara.

Pia alisema miundombinu ya Bandari ya Mtwara itakuwa na uwezo wa kupokea lita 25 milioni za mafuta lakini kwa kuanzia Juni wataanza na lita 10 milioni.

“Kampuni mbili tayari zimeshaagiza mafuta lita 10 milioni, wafanyabiashara wengine sasa waone Mtwara kama sehemu ya fursa na itapunguza msongamano," alisema.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )