Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, June 15, 2018

Afrika Yaanza Vibaya Kombe La Dunia......Misri, Morocco Zatandikwa Bao 1- 0

Dakika 90 zimemalizika kwenye Uwanja wa St, Petersburg kwa Iran kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Morocco.

Mchezo huo umeshuhudiwa huku milango ikiwa ni migumu zaidi kufungika kama ilivyokuwa kwa Misri dhidi ya Uruguay ambapo bao liliweza kupatikana kuelekea mwishoni mwa mchezo.

Katika dakika ya 90 zikiwa zimeongezwa tano mpira kumalizika, Morocco walijifunga kupitia kwa Aziz na kuweza kuwapa zawadi Iran ambao wameondoka kifua mbele kwa ushindi wa bao hilo pekee.

Morocco imekuwa timu ya pili kutoka Afrika kuweza kupoteza baada ya Misri kufungwa 1-0 na Uruguay kwenye dakika za mwisho za mchezo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )