Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, June 24, 2018

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Lapata Rais Mpya

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) leo Jumapili Juni 24, 2018 limemchagua Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Gervas Nyaisonga kuwa rais wa baraza hilo.

Askofu Nyaisonga aliyetangazwa leo katika misa  ya kumuweka wakfu Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga, Beatus Urassa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania mjini humo, amechukua nafasi ya Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa aliyemaliza muda wake.

Ngalalekumtwa amemtangaza Askofu Nyaisonga na kusema atatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )