Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, June 25, 2018

BAWACHA wasema katazo la mikutano ya hadhara Ni Pigo Kwa Wanawake

Baraza la Wanawake  Chadema (Bawacha) limesema uamuzi wa Serikali kupiga marufuku mikutano ya hadhara unarudisha nyuma juhudi za wanawake kufikia usawa wa asilimia 50 kwa wanawake kwa wanaume.

Kauli hiyo imetolewa jana Jumapili Juni 24, 2018 na makamu mwenyekiti wa baraza hilo, Hawa Mwaifunga wakati akizungumza na wanahabari katika mkutano wa kamati ya utendaji ya baraza hilo uliofanyika mjini hapa.

Mkutano huo wa siku mbili pamoja na mambo mengine unalenga kuwapa mafunzo, mbinu na ujasiri viongozi wa mikoa wa chama hicho.

Mwaifunga alisema wanawake wengi wamekuwa na hofu kutokana na uamuzi wa kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara, jambo ambalo linawafanya wanawake washindwe kujitosa katika siasa.

Alisema uamuzi huo umewanyima fursa Watanzania kuwasikiliza wanasiasa ili baadaye waje wafanye uamuzi wa kuwachagua wagombea wa chama kinachofaa.

“Kwa sasa ni kutishana na kukamatwa na kuwekwa ndani. Kipindi cha nyuma watu walifanya siasa za kistaarabu sana, ndiyo maana tuliwapata akina Halima Mdee (mwenyekiti Bawacha), Paulin Gekul (Babati Mjini (Chadema). Walipatikana baada ya kuonekana majukwaani,” alisema.

Katibu wa Bawacha,  Grace Tendega alisema wataendelea kupambana  licha ya kuwa wanaoonekana kufanya siasa majukwaani wanakamatwa.

Alisema baraza hilo limejipanga kuhakikisha majimbo sita yanayoongozwa na wabunge wanawake wa Chadema yanalindwa.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...