Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, June 25, 2018

Breaking News : Hiace Yagongana Na Lori La Mchanga Na Kuua Watu 14 Mkuranga

Watu 14 wamefariki dunia na wanne kujeruhiwa baada ya daladala walilokuwa wakisafiria kugongana na lori.

Ajali hiyo imetokea leo Juni 25 saa 10 alfajiri katika eneo la Dundani wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Dk Stephen Mwandambo amethibitisha vifo hivyo, amesema maiti za watu 14 zimepokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo.

"Ni kweli hili tukio limetokea alfajiri, tumepokea miili 14 na majeruhi wanne," amesema Dk Mwandambo.

Kati ya majeruhi hao, amesema mmoja hali yake ni mbaya na walikuwa wanahangaika kuokoa maisha yake.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )