Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 30, 2018

Dogo Janja Awachana Wanamponda kwamba Hana Sauti Kwa Mkewe Irene Uwoya

adv1
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Chande maarufu kama 'Dogo Janja' ambaye pia ni mume wa msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amedai katika ndoa yao yeye ndio mwanaume na mwenye sauti ya kutoa maamuzi ya jambo lolote tofauti na watu wanavyomfikilia.

Dogo Janja amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza  na kituo cha  EATV baada ya kuwepo kwa tetesi za kipindi kirefu zilizokuwa zinadai Janjaroo hana maamuzi yoyote katika ndoa yake kwa kuwa mwenye sauti ya kuamua jambo lolote ni mke wake Irene Uwoya.

"Ukiwa hauna maamuzi au sauti kwa mke wako wa halali ni kitu kizuri sana tofauti ukiwa hauna sauti kwa hawala. Mimi nina mtii mke wangu naye pia anafanya hivyo, kwenye ndoa yangu nina simama kama baba", amesema Dogo Janja na kuongeza;

"Watu wengi wanachukulia mambo kwa juu juu tu kwa mzaha, mimi nina sauti kwa mke wangu ninaweza kumwambia leo usitoke na huwa atoki au asifanye kitu fulani na akanisikiliza, 'so' sio kila jambo nitakalo mkataza basi nitangaze ila mpaka mke wangu akifanya jambo fulani mjue nina taarifa nayo na ninaelewa. Ndoa ni taasisi kubwa sana tofauti na watu ambao wapo tu mtaani wanatoa maamuzi yao bila ya kuelewa".

Kwa upande mwingine, Dogo Janja amedai watu wengi wamekuwa wanaongelea kuhusiana na ndoa yake kwenye mitandao ya kijamii bila ya kuwa na ufahamu wa aina yoyote juu ya taasisi hiyo ambayo ina uwanja mpana ndani yake.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )